Pastor Ajiua, alisema Mungu Hamskii Tena
Mchungaji Teddy Parker kutoka Georgia Marekani amejiua siku chache baada ya kuhubiri kanisani kwake kwamba Mungu hamsikii tena na wala ahisi muungane wake na Mungu tena.
" Najaribu kuomba, lakini nahisi Mungu anisikilizi tena, najitahidi kuhudumia lakini nahisi Mungu ahitaji kunitumia tena, zipo zama katika maisha ya binadamu ambazo Mungu kwa makusudi maalum hukuondoa, hakutoi ili ubaki peke yako ila hukufanya ukue na kujitambua zaidi" Alisema Teddy.
Parker, baba wa watoto wawili alijiua Jumapili iliyopita kwa kujipiga risasi kichwani na bastola yake baada ya kumaliza misa ya kwanza, watu walikuwa wakimngojea arudi kwa ajili ya misa ya pili na hakutokea, haikuwa kawaida na ndipo walipoenda kumuangalia walikuta ameshafariki.