Showing posts with label Fumanizi. Show all posts

YOUNG DEE AKAUNUSHA KUHUSU SKENDO YA KUFUMANIWA NA LULU WAKILA RAHA ZA UKUBWANI NDANI YA GARI




Juzi kupitia kwenye kipindi cha U-heard cha Clouds FM chini ya bwana Sudi Brown ama Gossip Cop kulikuwa na fununu kali iliyokuwa inamuhusu mwanadada wa Bongo Movies na mwimbaji wa muziki wa kizazi kipya Young D 'Young Dar es Salaam' kama mwenyewe anavyojiita baada ya wawili hao kukutwa kwenye gari wakifanya lile tendo linaloruhusiwa kufanywa mara baada ya mdada na mkaka kufunga ndoa.
Young D
                                                                                              

Kwa mujibu wa Sudi Brown 'Gossip Cop' wawili hao walikutwa maeneo ya Mbezi Beach ndani ya gari aina ya Hyundai ya mwanadada Lulu na polisi wa doria wakivunja amri hiyo iliyokatazwa na vitabu vyote vitakatifu kwa maana ya biblia, Quran na vitabu vingine vya dini ulimwenguni.

Habari zainasema baada ya wawili hao kukutwa eneo hilo na polisi walipelekwa pembeni gizani na kuongea na Polisi kabla ya wao kutokomea wasipojulikana na gari hilo.

Alipopigiwa simu mwanadada LULU alipokea na kukata muda mfupi na baadaye Young D alipopigiwa simu alitoa majiu ya utata kama alivyoongea mwenyewe kupitia kwenye kipindi cha U-heard cha Clouds Fm.
GPL

Read More »

Mwanaume Awagonganisha wanawake Airport saa 6 Usiku


MWANAUME mmoja aliyeelezwa kuwa ni tajiri mwenye nazo mjini, amezua tafrani na kusababisha timbwili la nguvu kwa dakika kadhaa baada ya kugonganisha wanawake wawili waliodaiwa kuwa chini ya miliki yake kwa wakati mmoja, subiri hapohapo tukujuze!

Mtiti huo uliovuta hisia za wengi ulichukua nafasi Ijumaa iliyopita, mishale ya saa sita na dakika zake usiku, pande za Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere ‘JNIA’ ambapo mwanaume huyo ambaye jina lake halikupatikana mara moja alitua na Ndege ya Shirika la Kenya.

ANGALIA SINEMA
Hali ya hewa ilikuwa ya kuridhisha kabisa katika eneo la uwanja wa ndege wakati paparazi wetu akiwa kwenye sehemu maalum ya kusubiria abiria wanaotua uwanjani hapo wakitokea nje ya nchi.
Paparazi wetu alikuwa akimsubiri mgeni wake lakini kama ilivyo kawaida ya wanakikosi cha Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’ alikuwa na zana zake za kazi kama kawaida.

Wakati wageni wakianza kutoka, ghafla zilisikika kelele pembeni mwa sehemu aliyokuwa paparazi wetu, akajiuliza kunani? Akaweka zana zake za kazi sawa kisha akajongea eneo la tukio.

VARANGATI LA NGUVU
Kamera za Risasi Mchanganyiko zilishuhudia wanawake wawili wakikunjana na kupigana makonde huku mmoja akimshutumu mwenzake kumwibia mumewe (haikujulikana kama ni wa ndoa). Alisema: “Wewe mpumbavu mwizi wa waume za watu, nitakukomesha leo. Si umezoea kuiba waume za watu? Sasa utanijua mimi ni nani?”

Mwanamke huyo aliyeonekana kuwa na jazba, alikuwa na watoto wake wawili waliovalia sare za shule ambao walikuwa wakimvuta na kumsihi aachane na ugomvi.

MSHANGAO NI HUU!
Sekeseke wakati likiendelea, yule mwanamke ambaye alikuwa akidai kuibiwa mumewe kwa muda mrefu na mwanamke huyo, watoto wake wawili walikuwa naye sambamba huku wakijaribu kumtuliza ingawa kiumri ni wadogo.
Mwanamke aliyedaiwa kuchukua mume wa mwenzake naye alikuwa na mtoto wake mmoja ambaye alikuwa akimvuta akitaka kumtoa mikononi mwa mwanamke aliyedaiwa kuwa mmiliki rasmi wa tajiri huyo.

Mshangao mkubwa ni kitendo cha watoto hao wote kuwa wamevaa sare za shule, tena zikionekana kuwa za shule moja – maswali yalikuwa mengi kuliko majibu!
“Hawa watoto sijui wamekuja na huyu jamaa? Maana wanaonekana kama wanasoma shule moja na wapo na vifaa vyao vyote vya shule. Hapa hata haileweki jamani,” alisikika dereva teksi mmoja aliyekuwepo eneo la tukio.

MAELEZO MENGINE
Mashuhuda walisema, awali tajiri yule wakati anatoka katika sehemu maalum ya abiria wanaoingia nchini, alikimbiliwa na mwanamke yule anayedaiwa kuwa kimada na kumpokea kisha kumbusu na kumpa pole kwa safari.

“Tatizo lilianzia pale yule mwanamke mwembamba mwenye nguo nyekundu alipoenda kumpokea jamaa. Alimfuata na kumkumbatia kisha akambusu, basi hapo tafrani ikatokea. Yule mke wa jamaa alikwenda haraka na kumvamia kisha kuanza kumpiga,” alisikika mmoja wa mashuhuda hao.

TAJIRI AWAZODOA WALIOMSHANGAA!
Wakati tafrani ile ikiendelea, mwanaume huyo aliwaingilia kati na kuwaamulia, jambo lililozidisha watazamaji wa sinema hiyo ya bure kushangaa.

Katika hali ya kushangaza, tajiri huyo aliwananga watu waliokuwa wakimshangaa akisema: “Sasa kipi cha ajabu? Ni mwanaume gani hapa ambaye hajawahi kufumaniwa? Haya ni mambo ya kawaida, endeleeni na shughuli zenu nitamaliza hii ishu mwenyewe.”

Juhudi za tajiri huyo kuwaachanisha zilizaa matunda, kwani zaidi ya kutumia nguvu, alionesha ‘uanaume’ wake kwa wanawake hao ambao walikubali kuachana na ugomvi huo ingawa kila mmoja alionekana kuwa na hasira na mwenzake.

Baadaye yule mwanamke aliyedaiwa kuwa ndiye mke halali wa tajiri yule, aliondoka naye wakiwa na watoto wao wawili, mwingine akaondoka na mtoto wake.



Read More »

JB afumaniwa na Mke wa Mtu Hotelini Dodoma



LILE sakata la madai kwamba, staa mkubwa wa filamu za Bongo, Jacob Stephen ‘ JB’ amenaswa akiwa na mke wa mtu mjini Dodoma limeingia katika sura tofauti baada ya habari yenyewe kujaa utata.

Habari za awali zilidai kuwa, tukio hilo lilitokea wikiendi iliyopita katika hoteli moja (jina lipo) iliyopo mjini Dodoma ambapo JB alikutwa na mke huyo wa mtu aliyetambulika kwa jina moja la Sarah.
Kwa mujibu wa mwanaume aliyedai kuwa ni mume wa Sarah aitwaye Rama (jina moja), alifuatilia nyendo za mkewe huyo kwa saa kumi na mbili siku ya tukio na mawasiliano yake ambapo kwa muda mrefu alikuwa akiwasiliana na JB ambapo walipanga kukutana katika hoteli hiyo usiku.
Saa tatu usiku, Rama alifika ndani ya hoteli hiyo na kuingia kwenye chumba alichokuwa amelala JB na mwanamke huyo ambapo aligonga mlango kwa muda mrefu baadaye sana ndipo ukafunguliwa.
Baada ya mlango kufunguliwa, kwa mujibu wa mume wa Sarah,  JB alipokea  kipigo cha haja kutoka kwa mwanaume huyo ambapo wahudumu wa hoteli na polisi waliokuwa wanafanya doria katika shoo ya Jahazi iliyokuwa ikiendelea kwenye ukumbi wa hoteli hiyo  waliingilia kati kumuokoa JB na walipelekwa Kituo cha Polisi cha Area D ambapo maelezo yalichukuliwa na kutakiwa warudi kesho yake.
Mwanaume huyo alisema kuwa kesho yake waliporudi polisi walimshinikiza akubali yaishe ambapo walilazimishwa kuelewana.
Mume huyo akasema hakurudi nyumbani tangu siku hiyo mpaka juzi hata hivyo akasema:
 “Mimi simuhitaji tena japokuwa ana mimba ya miezi minne na sina uhakika kama ni ya kwangu kwani tabia zake sizielewi bora niachane  naye maana tulikuwa wachumba hatujafunga ndoa.”

HUYO ALIKUWA MUME, JB SASA
Mapaparazi wetu walifanikiwa kumuweka mtu kati JB ambapo baada ya kumuuliza kilichotokea, alisema:
“Mimi nifumaniwe! Hivi inawezekana kweli? Mna uthibitisho au ushahidi wowote? Yule msichana alikuwa klabu, akachukua namba yangu. Si yeye tu, mashabiki wengi waliniomba namba siku hiyo.
“Ulikuwa usiku akarudi klabu, mimi nilikuwa hotelini, akanipigia na kusema anataka kuniona ana shida ya kisanii.
“Hata alipokuja sikuwa nimefunga mlango, akaingia na bado mlango ulikuwa wazi. Muda mfupi baadaye akaingia huyo bwana akiwa peke yake na kusema amenifumania.
“Hivi jamani, kweli unakwenda kumfumania mkeo upo peke yako? Kwanza hatari! Nilipoona anachachamaa kwa madai hayo, nilitoka nje, huyo anayesema mkewe naye akaondoka lakini alikuwa akisema mbele yake kwamba hajaolewa.
“Kule nje niliwaambia wenye hoteli, wakaamua kuita polisi maana alikuja kunifanyia fujo. Sijui nini kiliendelea, lakini ukweli ni kwamba sikufumaniwa.”
Sarah alipopatikana hewani juzi  alisema hajafumaniwa na huyo anayedai ni mumewe ni mpenzi wake tu. Alidai kama kufumaniwa angekutwa akiwa hana nguo.
Staa mkubwa wa filamu za Bongo, Jacob Stephen ‘ JB’.

Habari za awali zilidai kuwa, tukio hilo lilitokea wikiendi iliyopita katika hoteli moja (jina lipo) iliyopo mjini Dodoma ambapo JB alikutwa na mke huyo wa mtu aliyetambulika kwa jina moja la Sarah.
Kwa mujibu wa mwanaume aliyedai kuwa ni mume wa Sarah aitwaye Rama (jina moja), alifuatilia nyendo za mkewe huyo kwa saa kumi na mbili siku ya tukio na mawasiliano yake ambapo kwa muda mrefu alikuwa akiwasiliana na JB ambapo walipanga kukutana katika hoteli hiyo usiku.
Saa tatu usiku, Rama alifika ndani ya hoteli hiyo na kuingia kwenye chumba alichokuwa amelala JB na mwanamke huyo ambapo aligonga mlango kwa muda mrefu baadaye sana ndipo ukafunguliwa.
Baada ya mlango kufunguliwa, kwa mujibu wa mume wa Sarah,  JB alipokea  kipigo cha haja kutoka kwa mwanaume huyo ambapo wahudumu wa hoteli na polisi waliokuwa wanafanya doria katika shoo ya Jahazi iliyokuwa ikiendelea kwenye ukumbi wa hoteli hiyo  waliingilia kati kumuokoa JB na walipelekwa Kituo cha Polisi cha Area D ambapo maelezo yalichukuliwa na kutakiwa warudi kesho yake.
Mwanaume huyo alisema kuwa kesho yake waliporudi polisi walimshinikiza akubali yaishe ambapo walilazimishwa kuelewana.
Mume huyo akasema hakurudi nyumbani tangu siku hiyo mpaka juzi hata hivyo akasema:
 “Mimi simuhitaji tena japokuwa ana mimba ya miezi minne na sina uhakika kama ni ya kwangu kwani tabia zake sizielewi bora niachane  naye maana tulikuwa wachumba hatujafunga ndoa.”

HUYO ALIKUWA MUME, JB SASA
Mapaparazi wetu walifanikiwa kumuweka mtu kati JB ambapo baada ya kumuuliza kilichotokea, alisema:
“Mimi nifumaniwe! Hivi inawezekana kweli? Mna uthibitisho au ushahidi wowote? Yule msichana alikuwa klabu, akachukua namba yangu. Si yeye tu, mashabiki wengi waliniomba namba siku hiyo.
“Ulikuwa usiku akarudi klabu, mimi nilikuwa hotelini, akanipigia na kusema anataka kuniona ana shida ya kisanii.
“Hata alipokuja sikuwa nimefunga mlango, akaingia na bado mlango ulikuwa wazi. Muda mfupi baadaye akaingia huyo bwana akiwa peke yake na kusema amenifumania.
“Hivi jamani, kweli unakwenda kumfumania mkeo upo peke yako? Kwanza hatari! Nilipoona anachachamaa kwa madai hayo, nilitoka nje, huyo anayesema mkewe naye akaondoka lakini alikuwa akisema mbele yake kwamba hajaolewa.
“Kule nje niliwaambia wenye hoteli, wakaamua kuita polisi maana alikuja kunifanyia fujo. Sijui nini kiliendelea, lakini ukweli ni kwamba sikufumaniwa.”



Sarah alipopatikana hewani juzi  alisema hajafumaniwa na huyo anayedai ni mumewe ni mpenzi wake tu. Alidai kama kufumaniwa angekutwa akiwa hana nguo.

GPL.


Read More »

Atakiwa kukusanya Face Book Like 10,000 ali asamehewe na Mkewe Baada ya Kumsaliti



Sonya Gore aliyetengana na Mumuwe baada ya miezi 10 ya ndoa yao mnamo December 2010  kutokana na Tabia endelevu ya mumewe huyo kuisaliti ndoa yao ameamua kumpa Mtiani mwanaume wake ili aweze kumsamehe na kuendelea kuishi wote katika maisha ya ndoa.

"Ikiwa ananipenda basi ananipenda na hana jinsi ispokuwa kutekeleza masharti yangu" alisema Sonya. Katika kulifanya hilo, mume huyo aliamriwa achukue karatasi na andike kwa mkono wake kukiri kosa lake kisha kujipiga picha nalo huku akibembeleza apewe hizo likes 10,000.

Mpaka sasa Tangazo hilo la Ivan Lewis(Mumewe) limepata likes 6,500 tu hivyo bado kuna safari ndefu kidogo.

Wife agrees to take cheating husband back if he gets 10,000 likes on Facebook (PHOTOS)


Read More »

Sakata na Mchungaji Mwingira kuzaa na mke wa Mtu, Kikwete Aingilia Kati.


RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, ameingilia kati sakata la Mtume na Nabii Josephat Mwingira kudaiwa kuzaa na mke wa mtu. 

JK, aliingilia kati sakata hilo baada ya mume wa mtu, Dk. William T. Morris, kukamatwa na maofisa wa uhamiaji kisha kutakiwa kufukuzwa nchini kutokana na kile kinachodaiwa ni ‘shinikizo la mtu mwenye nguvu’.
Habari ambazo Uwazi limezithibitisha ni kwamba baada ya Dk. Morris kufungua mashtaka akimtuhumu Mwingira kuzaa na mkewe, Dk. Philis Nyimbi, alikamatwa na maofisa wa uhamiaji kisha kupewa hati ya kutimuliwa nchini.
Uwazi limebaini kuwa JK ndiye aliyezuia hati hiyo na mpaka sasa, Dk. Morris, raia wa Liberia, yupo nchini akiendelea na harakati zake za kusaka haki kisheria kuhusiana na madai yake hayo.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete.
JK ALIMFIKIAJE?
Inaelezwa kuwa wakati Dk. Morris alipokamatwa, alitokea msamaria mwema (jina tunalo) anayejua ‘njia za kupita’ kufika Ikulu ambaye alimfikishia JK mkanda mzima wa sakata hilo la Mwingira.

“… (anataja jina la msamaria mwema), alimwambia JK kuwa nchi inaelekea katika aibu, Dk. Morris ni mtu anayetambulika Umoja wa Mataifa (UN) hasahasa Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO).
“JK baada ya kusimuliwa kila kitu, alichokifanya ni kuingilia kati na kuzuia Dk. Morris asifukuzwe nchini,” kilisema chanzo chetu na kuongeza:


Mtume na Nabii Josephat Mwingira.
“Vilevile JK aliomba namba ya Dk. Morris kisha alimtumia SMS na baadaye wakaongea, akamhakikishia yupo salama nchini lakini kuhusu madai yake kuhusu mkewe, aendelee kufuata sheria.”
HATI YAKE BADO INASHIKILIWA NA UHAMIAJI
Habari zaidi zinaweka kweupe pamoja na JK kuzuia Dk. Morris asitimuliwe nchini, bado maofisa wa uhamiaji Mkoa wa Pwani, wanashikilia hati yake ya kusafiria (passport) mpaka leo.

Dk. Morris alipoulizwa kuhusu hilo, alikiri: “Ni kweli wanaishikilia. Niliwaomba wale maofisa wanipe nyaraka inayoonesha passport yangu wanaishikilia. Niliogopa wanaweza kunigeuka. Waliniandikia, kwa hiyo sina wasiwasi.”

Cheti cha ndoa ya Dk. Morris na mkewe Dk. Philis.
SAKATA LENYEWE LIPOJE
Toleo lililopita la gazeti hili, tuliandika habari yenye kichwa Mume: Mwingira amezaa na mke wangu.
Katika habari hiyo, gazeti hili lilisimamia tuhuma zilizofunguliwa na Dk. Morris kwenye Kituo cha Polisi Kati (Central), Kibaha, Pwani, akidai Mwingira amezaa na mkewe.

Shauri hilo lilifunguliwa kwa kichwa JALADA LA UCHUNGUZI, nambari KBA/PE/20/2011, mtuhumiwa akiwa Josephat Mwingira.
Habari yetu iliyopita, mke wa Dk. Morris, Dk. Philis, alidai alizaa nje ya ndoa baada ya kutekelezwa na mumewe, ingawa alikataa kumtaja mwanaume aliyezaa naye.

Zaidi ya hapo, Dk. Philis alisema Dk. Morris hakuwa mwaminifu kwenye ndoa, kwani alidiriki kumsaliti kwa binti mwenye umri chini ya miaka 18 ambaye wao kama mke na mume, wangeweza kumzaa.
Mtoto wa Nabii Mwingira aliyezaa na Dk. Philis.

DK. MORRIS NA MWANDISHI WETU
Katika kumchimba zaidi Dk. Morris, mwandishi wetu alifanya naye mahojiano kama ifuatavyo;
MWANDISHI: Ni kweli ulimtelekeza mkeo ndiyo maana akaamua kusaliti na kuzaa nje ya ndoa?
DK. MORRIS: Si kweli hata kidogo, amenisingizia, naomba amuogope Mungu.
MWANDISHI: Una ushahidi wowote kuwa ulikuwa unamjali mkeo?

DK. MORRIS: Ushahidi upo wa kutosha. Anazungumzia kipindi cha kuanzia mwaka 2006 mpaka 2011, ni kipindi ambacho nilikuwa naishi Marekani kikazi WHO.
Kipindi hicho, nilikuwa namtumia mke wangu dola za Kimarekani 2500 (zaidi ya shilingi 4,000,000) kila baada ya wiki mbili lakini kuna wakati nilikuwa nampa zaidi ya hizo.

Gazeti hili lilioneshwa nakala ya karatasi za kibenki zikionesha jinsi alivyokuwa akimuingizia fedha mkewe aliyekuwa na akaunti katika Benki ya Standard Chartered Moshi (namba ya akaunti tunaihifadhi), yeye akiwa Marekani akitumia Bank of America kuanzia mwaka 2006.
MWANDISHI: Hebu niambie, Dk Philis bado ni mke wako? Yeye anasema wewe siyo mumewe.
DK. MORRIS: Ni mke wangu halali wa ndoa takatifu. Nilifunga naye ndoa katika Kanisa la St Alban, Dar Desemba 23, 2001, nikiwa na umri wa miaka 39 na yeye (mkewe) akiwa na miaka 30.

Ndoa hiyo niliigharamia sana tangu mavazi ya wapambe wangu na wa mke wangu. Ilikuwa siku ya furaha kabisa. Sikupenda wakwe zangu wapate shida.
MWANDISHI: Ukiwa Marekani ulipata habari zozote za kuwa mkeo ni mjamzito au kajifungua?

DK. MORRIS: Hapana, sikuwa na habari kabisa juu ya jambo hilo na ndiyo maana nilikuwa nikimtumia fedha za kutosha.
Kuna siku moja aliniambia anataka kwenda kufanya utafiti Afrika Kusini, akawa  anataka dola 2500 siku hiyohiyo aliyoniambia. Nilimwambia taratibu za fedha Marekani ni ngumu. Nilikwenda ofisini kwangu nikaomba malipo ya awali ya mshahara wangu, nikamtumia dola za Kimarekani 3,000 (shilingi milioni 4.8 kwa cheji ya sasa).

MWANDISHI: Uliporejea Tanzania, ilikuwaje ukajua mkeo amezaa nje ya ndoa?
DK. MORRIS: Nakumbuka usiku mke wangu alianza kulia. Nilishangaa nikamuuliza kwa nini unalia, akanijibu kwamba anaomba nimsamehe kwa sababu amezaa nje ya ndoa.
MWANDISHI: Baada ya kusikia hivyo ulijisikiaje?

DK. MORRIS: Niliishiwa nguvu kabisa, nikamuuliza kwa nini amefanya usaliti huo? Nilimuuliza ni nani amempa mimba, akaniambia ni mwanaume mmoja injinia ambaye alidai yupo Marekani kwa wakati huo.
MWANDISHI: Hayo ulikuwa unamuuliza mkiwa wapi Dar au Kibaha?

DK. MORRIS: Tulikuwa Moshi, nikiwa Marekani mke wangu aliniambia yupo Moshi anachukua shahada ya pili (Master) ya udaktari, na nilikuwa namtumia fedha za pango la nyumba, lakini pale nilimkuta hotelini, kesho yake tukarudi Dar.
MWANDISHI: Baada ya kufika Dar mambo yalikuwaje?
DK. MORRIS: Mke wangu aliniambia kuwa ni lazima nimsindikize kwa Nabii Mwingira ili akaombewe kwa ushetani alioufanya wa kuzaa nje ya ndoa.

MWANDISHI: Ulikubaliana naye?
DK. MORRIS: Nilimkubalia tukaenda kwa sababu wakati huo nilikuwa sijajua kuwa yeye ndiye mbaya wangu. Tulimkuta na akatukaribisha ofisini kwake.
MWANDISHI: Mambo yakawaje?

DK. MORRIS: Mwingira alituombea, wakati akituombea Mwingira mwenyewe alilia sana.
MWANDISHI: Ukaja kumtuhumu vipi tena Mwingira kuwa amezaa na mkeo?
DK. MORRIS: Subiri kwanza, kesi ikishakuwa mahakamani yote yatakuwa wazi. Nitataka pia tupimwe kila kitu, DNA  pamoja na Ukimwi.

MWANDISHI: Vipi madai ya wewe kutimuliwa nchini?
DK. MORRIS: Namshukuru sana Rais Kikwete, ni kiongozi mzuri, alinisaidia sana. Namuamini, nampenda na nawaomba Watanzania wampende kiongozi huyu, ni mpenda haki.

MWINGIRA BADO SHIDA
Jitihada za waandishi wetu kumpata Mwingira bado hazijazaa matunda, kwani kila njia inayotumika, wasaidizi wake hawataki kabisa kiongozi huyo wa Kanisa la Efatha, afikiwe na kuhojiwa kuhusu madai haya.
Hata hivyo, Uwazi halijakata tamaa, litaendelea kumsaka mpaka apatikane na kujibu tuhuma hizo.


Chanzo:Globalpublishers

Read More »

Gesti Bubu Nyingine Inayofuga Machangudoa Yabainika


MZEE mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Abdullahimu Mnami (48) amenaswa akiendesha gesti bubu kinyume cha sheria za nchi.

Baadhi ya wananchi walionaswa katika msako wa biashara haramu ya ukahaba. Pichani ni wauzaji na wanunuzi.
Tukio hilo lilitokea Oktoba 26, mwaka huu maeneo ya Tuangoma jijini Dar, baada ya waandishi wetu kuzinyaka taarifa hizo na kuzifikisha kwa mwenyekiti wa serikali ya mtaa huo, Chande Mohammed aliyefika eneo hilo na polisi.
Awali, ili kujiridhisha, mmoja wa mapaparazi wetu alijifanya mteja na kufika katika gesti bubu hiyo, kisha kupangisha chumba kwa malazi ya siku moja kwa malipo ya shilingi 3000 tu lakini pasipo kuandikisha mahali popote.
Mmiliki wa gesti bubu inayotumika katika biashara haramu ya ukahaba baada ya kutiwa nguvuni.
Akizungumza na waandishi wetu mbele ya maaskari na mwenyekiti, mzee huyo alisema alishindwa kuisajili gesti yake kwa kuwa haikuwa na viwango vinavyokubalika na manispaa (ya Temeke).
“Ningefuata utaratibu, manispaa isingeniruhusu kutokana na ubora wa vyumba vyenyewe, kama mnavyoona. Pia njaa tu jamani ndiyo imenifanya nianzishe gesti hii,” alisema mzee Abdullahim.
Eneo la ndani ya gesti bubu inayotumika kwa ukahaba.
Hata hivyo mwenyekiti wa mtaa huo, alisema kuwa mzee huyo ana kesi ya kujibu kwa kukiuka taratibu za kibiashara zilizowekwa na halmashauri na kumuamuru aifunge gesti hiyo mara moja huku akiahidi kumpeleka Baraza la Kata kwa ajili ya masikilizano ya awali.
Timu yetu iliwaachia msala wao na kuendelea na oparesheni nyingine ambapo walifanikiwa kuwanasa machungudoa wakijiuza jirani na mtaa huo huku ikielezwa kuwa, wateja wa madadapoa hao hupelekwa katika gesti bubu ya mzee huyo kwa vile ni bei poa.
Wateja na wafanyabiashara haramu ya ukahaba wakiwa chini ya ulinzi baada ya kunaswa.
GPL

Read More »

Mke anaswa Akijivinjari na Hawara Ndani ya Chumba cha Mumewe, Angalia Yaliyomkuta Mgoni huyo!!!




TIMBWILI zito limeibuka baada ya mwanaume aliyetajwa kwa jina moja la Samora kumnasa ‘live’ mkewe Hadija akimsaliti kwa kuvunja amri ya 7 (usizini) na hawara ndani ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, tena kwenye chumba chao, Ijumaa lina ishu kamili.

Mshangao: mtuhumiwa akikodoa macho baada ya kunaswa live na mke wa mtu chumbani kwa mwenye mali.
Habari kutoka chanzo cha uhakika kilitonya kuwa Samora na Hadija ni wanandoa waliooana Bomani pale Magomeni, Dar, mwaka 2009 na katika ndoa yao wamebahatika kupata mtoto mmoja wa kiume.
Tukio hilo la fumanizi lilijiri maeneo ya Kinondoni-Kwamsisiri, Dar nyumbani kwa wanandoa hao, majira ya saa 1:00 usiku, Julai 29, mwaka huu.
Aibu: mtuhumiwa akijaribu kuficha sura yake baada ya fumanizi hilo.
NDOA YATUMBUKIA NYONGO
Habari zilieleza kuwa mwanzoni mwa mwaka huu, ndoa ya wawili hao ilitumbukia nyongo na kuingia kwenye mgogoro ambapo pamoja na kuweka mambo sawa, waliendelea kukwaruzana mara kwa mara.
Mshangao: Nisameheni jamani!
CHANZO NI NINI?
Ilidaiwa kuwa chanzo cha wawili hao kuhitilafiana ni kutokana na mwanaume kumtuhumu mkewe kutoa tunda nje ya ndoa.
Ikasemekana kuwa baadaye wapambe walimfuata Samora na kumtonya kuwa mkewe amekuwa na uhusiano wa kimapenzi na kidume mwingine nje ya ndoa yao ndiyo maana amekuwa akimletea nyodo ‘mapichapicha’.
Iliendelea kudaiwa kuwa baada ya ndoa kutibuka, Samora alikuwa mnyonge na mwenye msongo wa mawazo hivyo ikabidi aikimbie nyumba kwa muda na kwenda kwa wazazi wake.
Ilisemekana kuwa, Samora alirejea nyumbani huku akifanya uchunguzi wa nguvu akiwatumia majirani kumpatia taarifa kuhusu kila mwanaume aliyeingia na kutoka nyumbani kwake yeye akiwa hayupo.
Bwana Samora akiwa na mkewe Hadija siku ya harusi yao.
KUMBE NI RWEKAZA
Uchunguzi wa Samora ulibaini kuwa, Hadija alikuwa ‘akibanjuka’ nje ya ndoa na mwanaume aliyetajwa kwa jina moja la Rwekaza ambaye ni mfanyakazi serikalini.
Habari za kina zilisema kuwa, Samora alitonywa kwamba jamaa alikuwa akitimba na gari aina ya Suzuki Swift 1.3 na siku nyingine alikuwa akilala hadi asubuhi bila tone la soni kuwa Hadija ni mke wa mtu.
Samora na Hadija wakiwa na wapambe wao siku ya harusi.
SAMORA AJIPANGA
Baada ya kupata uhakika huo ndipo Samora akajipanga kwa kuwatafuta vijana wa mtaani ili Rwekaza atakapofika nyumbani hapo kulala na mkewe wamvamie na kumfanyizia.
Mshikemshike: Samora (wa tatu kushoto) na wapambe wake wakitaka kumshushia kichapo mtuhumiwa.
RWEKAZA MTEGONI
Bila kufahamu kuwa anasubiriwa kwa hamu majira yaa saa 1:00 usiku, Rwekaza huyooo, akatinga nyumbani hapo na moja kwa moja akafikia chumbani kama kawaida yake.
Wakiwa chumbani, ilidaiwa kuwa waliendelea na mambo yao huku Rwekaza akiwa tumbo wazi na suruali yake amefungua zipu huku Hadija akiwa amesaula na kubaki na ‘kufuli’, kisha akajifunga khanga moja.
Hasira: Samora (kushoto) akimkunja mwizi wake baada ya kumfumania.
FUMANIZI KABANG’
Katika fumanizi hilo, Samora alitinga chumbani humo akiwa ameambatana na kundi la vijana kibao ambao walikuwa na lengo moja tu, kumfanyia kitu mbaya Rwekaza.
Wakiwa chumbani, kuliibuka bonge la timbwili baada ya Samora kumshuhudia mwenza wake aliyekula kiapo cha kutotengana naye akisaliti ‘laivu’ penzi lao.
Baada ya kuona machafuko makubwa ya hali ya hewa chumbani, mwanahabari wetu aliwataarifa polisi katika Kituo cha Kwamsisiri ambao walifika maeneo hayo na kufanya kazi kubwa na nzuri ya kuepusha balaa au mauaji kwa kuwa Samora alikuwa na hasira kali.
Albamu ikionyesha picha walizopiga Samora na mkewe Hadija wakati wakisaini kitabu cha ndoa.
KWELI NI MKE WA NDOA?
Ili kuthibitisha kuwa ni mkewe wa ndoa, Samora alizama kabatini na kuchomoa cheti cha ndoa na picha walizopiga siku ya ndoa yao zikiwaonesha wakiwa na tabasamu la ‘mimi na wewe milele’ kabla ya shetani ‘kufanya yake’ kwenye unganiko lao.
Wananchi wakiwa nje ya nyumba alipofumaniwa bwana Rwekaza.
MAJIRANI
Kwa mujibu wa majirani, tukio hilo liliwasikitisha wengi huku wakiamini kabisa kuwa ni nadra matukio ya mafumanizi kutokea katika kipindi cha mfungo.
“Jamani hata Mwezi Mtukufu? Ni aibu sana kwa mke kuingiza mwanaume mwingine kwenye chumba cha mumewe. Kweli hili fumanizi ni kiboko,” alisikika mmoja wa majirani hao walioshuhudia tukio hilo muda mfupi baada ya kufuturu.
Gari la mtuhumiwa aina ya Suzuki Swift 1.3 likiwa nje ya nyumba alipofumaniwa.
SAKATA LINAENDELEA
Hadi gazeti hili linaondoka eneo la tukio wahusika wote walikuwa kituoni hapo hivyo tunaendelea kulifuatilia sakata hilo kwa karibu sana na pia kuwapata wahusika wazungumzie kilichojiri.

CHANZO: GPL

Read More »

Mwanaume Akatwa Miguu baada ya Kufumaniwa na Mke wa Mtu



Na Mwandishi Wetu, Kilosa
ALI Omar, mkazi wa Kijiji cha Mabana, wilayani Kilosa, Mkoa wa Morogoro anashikiliwa na polisi kwa kosa la kumkata miguu Said  Iddi kwa kumtuhumu kumfumania na mkewe aliyejulikana kwa jina la mama Ali, mkanda mzima upo mikononi mwa Amani.


Mke wa mtu sumu: Said  Iddi akiwa chini baada ya kukatwa miguu na Ali Omar.
Tukio hilo la kikatili lilijiri Julai 15, mwaka huu wakati Said na mama Ali walipokuwa ndani ya nyumba ya Ali iliyopo kijijini hapo.
MANENO YA SHUHUDA
Akizungumza na mwandishi wetu, shuhuda mmoja ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja alisema Said alifumaniwa ndani ya nyumba asubuhi akiwa na mke wa Ali baada ya kuwekewa mtego ambao ulimnasa vizuri.
“Ali alipewa habari na kijana mmoja aitwaye God kwamba mkewe si mwaminifu katika ndoa, akamwongezea kuwa anatoka kimapenzi na Said. Ndipo Ali na mnyetishaji wake huyo walipopanga kumfumania jamaa,” alisema shuhuda.
Chini ya ulinzi: Mwenye mali, Ali Omar (kati) akiwa chini ya ulinzi baada ya kumkata Said.
Aliongeza kudai kuwa, Said ni msimamizi wa mashamba ya Ali kijijini hapo na kwamba God ni mtoto wa mwenye nyumba ambayo Ali amepanga kijijini hapo.
MPANGO WA FUMANIZI
Habari zinapasha kuwa mara baada ya mnyetishaji kutoa taarifa za usaliti huo, Ali alimtafuta  ‘baunsa’ ambaye jina lake halikuweza kujulikana mara moja na wakaweka mtego kwa kujificha karibu na nyumba hiyo ambayo Said angeingia ili kuivunja amri ya sita ya Mungu.
Umbea kazi: Kijana aitwaye God (kulia) aliyetoa taarifa kwa Ali naye akiwa chini ya ulinzi.
Katika kufanikisha mtego huo, mmbeya huyo alipewa jukumu la kuhakikisha nyendo za Said na mama Ali siku hiyo zinarekodiwa mpaka kuingia ndani ya nyumba hiyo na kumtaarifu Ali ambaye siku hiyo alimuaga mkewe kwamba amesafiri.

SAID ATINGA NYUMBANI KWA ALI
Habari zinasema mtoboa siri huyo alimwambia Said kuwa Ali amesafiri na ndipo jamaa akafunga safari kwenda kwa mama Ali kwa nia ya kujivinjari licha ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ukifikia katikati.
Mwanamke hutulii?: Mke wa Ali Omar naye akipelekwa polisi baada ya tukio hilo.
Habari zinadai mara baada ya kufika kwa Ali, Said aliingia ndani ya nyumba bila kujua kwamba mwenye mke alikuwa amejificha jirani akisubiri mtego unase.
Inasemekana Said akiwa ndani, Ali na baunsa wake waliibuka kwa kutaarifiwa na God na kumnasa jamaa huyo huku akidai ni mgoni wake. Alimuuliza maswali kadhaa, yakiwemo haya:
“Umekuja kufanya nini ndani ya nyumba yangu? Kwa nini umekaa na mke wangu?”
Habari zinasema Said alijibu hakuona ubaya kwa kuwa yeye ni mwangalizi wa mashamba ya mwanaume huyo hivyo anaweza kuingia ndani kwake wakati wowote.
Said  Iddi akiwa amezungukwa na wananchi baada ya kukatwa miguu.
MWENYE MKE ATIBUKA NA MAJIBU, AMWAGA DAMU
Jibu hilo lilidaiwa kumtibua Ali na ndipo yeye na baunsa wake wapomfunga kamba miguuni Said na kuanza kumkata kwa panga mguu mmoja kisha kuugeukia wa pili.
Said alipiga mayowe yaliyowafanya wanakijiji kukimbilia eneo la tukio kwa lengo la kujua kulikoni ambapo walimkuta Said akiwa anavuja damu na sehemu ya nyuma ya miguu ikiwa nyanga’nyang’a.
Said akipelekwa kwenye difenda.
MWENYE MKE AKIMBIA, ANASWA
Ali, God na baunsa walikimbia eneo hilo. Baadhi ya wanawake walitumia khanga zao kuifunga miguu ya Said kwa lengo la kujaribu kuzuia damu isiendelee kumwagika. Said alikuwa akilia sana.
“Wanakijiji walichukizwa sana na ukatili uliofanywa na Ali, hivyo wakaanza kumsaka na kumkamata kichakani akiwa amejificha pamoja na God. Alipewa mkong’oto kwa lengo la kutaka kumuua, lakini viongozi wa kijiji walisihi asiuawe bali afikishwe kwenye kituo cha polisi,” alisema shuhuda.
...Akiingizwa ndani ya difenda.
MKE, MUME, MMBEYA WAFIKISHWA POLISI
Polisi wa Kituo cha Dumila waliitwa na kumchukua Said, Ali na God kwa kutumia gari aina ya Land Rover lenye namba za usajili T 750 AAJ. Mke wa Ali yeye alipelekwa polisi kwa pikipiki.
Walipofika kituoni, Said alipewa fomu ya matibabu ya polisi (PF 3) na kupelekwa Hospitali ya Wilaya ya Kilosa kwa matibabu.
“Pale hospitali Said alishonwa miguu yote lakini madaktari wakaamua ahamishiwe katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro kwa matibabu zaidi,” alisema shuhuda huyo.
Bwana Said akiwa ndani ya difenda.
ANAWEZA ASITEMBEE TENA
Akaongeza: Daktari mmoja alisema haamini kama jamaa (Said) atatembea tena kwa sababu zana iliyotumika kumkata ilifika hadi kwenye mishipa ya nyuma ambayo ndiyo humfanya binadamu aweze kusimama na kutembea.
Said akishonwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kilosa.
BAUNSA ASAKWA
Afisa mmoja wa polisi kituoni hapo ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini kwa kuwa si msemaji, alisema wanaendelea kumsaka baunsa aliyeshirikiana na Ali kumkata miguu Said.
...Said akizidi kupatiwa huduma.




 SOURCE: GPL

Read More »

Mke Amfuma Mumewe na "Shostito" wake Guest House, Amshushia Kipondo Heavy!!

-->





Kweli Mke wa Mtu Sumu na Mume wa Mtu maziwa, baada ya tetesi za muda mrefu kwamba shoga yake ndiye anayemtibulia ndoa yake hatimaye ukweli umejidhihirisha baada ya Mke kumfuma Mumewe wakiwa na Besti wake huyo ambaye mbali na kusoma pamoja hadi Field walifanya pamoja lakini bado akamtenda mwenzie visivyo.
Baada ya Fumanizi hilo mke aliamua kuwapigia mashoga wengine waliokuwa karibu ili washirikiane kumshushia kipondo mwizo huyo.

Read More »

Baada ya Fumanizi, Walazimishwa kufanya Mapenzi Hadharani.

Ama kweli mke wa mtu sumu, Siku za hivi karibuni huko, Nigeria karibu na cho kikuu cha Anambra, ilitoka hukumu ya aina yake baada ya mume kumfuma mkewe akivunja amri na mpenzi wa nje. Baad ya fumanizi hilo mume mtu akiwa na wenzake walimtoa jamaa huyo na mkewe hadi uwanjani huku wakiwalazimisha waendelee na kitendo chao hadharani.

Hata hivyo mume hakuweza kukaa na kuangalia badala yake alirudi nyumbani na kutupa vitu vya mwanamke huyo nje.


Video hii pia ilikuwepo you tube lakini ilionfolewa baada ya kuonekana inapingana na Terms of Service(Tos)



Read More »

Sista Aliyefumaniwa Atozwa Faini ya Laki Saba

MAHAKAMA ya Mwanzo mjini hapa, imemtia hatiani aliyekuwa mtawa wa Shirika la Kitawa la Kanisa Katoliki Jimbo la Sumbawanga, Sista Yasinta Sindani, kwa kufumaniwa na mume wa mtu na kuamriwa kumlipa fidia ya Sh 700,000 mlalamikaji.
Katika kesi ya msingi ya madai, mlalamikaji Asteria Mgabo alimtaka Sista Yasinta amlipe Sh milioni 3 baada ya kumfumania na mumewe wa ndoa, Martin Msangawale (39) ambaye pia ni mkazi wa mjini hapa.
-->
Sista huyo ambaye ni daktari katika Hospitali ya Mkoa wa Rukwa mjini hapa, kwa sasa anaishi nje ya nyumba ya utawa eneo la Kantalamba.
Katika hati ya awali ya madai, inadaiwa mshitakiwa alifumaniwa na Asteria akiwa na mumewe Msangawale wakiwa kwenye nyumba ya kulala wageni ijulikanayo kwa jina la Chipa iliyopo eneo la Katandala mjini hapa, Desemba 24 mwaka jana majira ya saa 7 usiku ikiwa ni siku ya mkesha wa Sikukuu ya Krismas.
Akisoma hukumu hiyo juzi, hakimu wa mahakama hiyo, Jaffar Mkinga alisema kuwa ushahidi uliotolewa na mlalamikaji ulikuwa mzito wenye kuondoa shaka zote kuwa mdaiwa alitenda kosa hilo tofauti na utetezi uliotolewa na mdai kuwa ulikuwa dhaifu.
Awali katika utetezi wake mdaiwa aliiambia mahakama hiyo kuwa kwanza alikuwa hajui kuwa Martin alikuwa mume wa mtu na kukiri mbele ya mahakama hiyo kuwa alimweleza kuwa hana mke hivyo alimwomba amuoe.
Lakini Hakimu Mkinga alipinga utetezi huo kwa sababu usiku huo wa mkesha wa Krismas mwaka jana, saa saba na robo usiku, mlalamikaji akiongozana na mwenyekiti wa mtaa wakiwa na mashahidi wengine watatu, walimkuta mdaiwa na Martin wakitoka katika moja ya vyumba katika nyumba ya kulala wageni ya Chipa, akasainishwa.

“Kama hukufahamu kuwa Martin alikuwa hana mke ilikuwaje ukakubali kusaini karatasi hiyo ya fumanizi iliyoandaliwa na mwenyekiti huyo?” alihoji hakimu, akamhukumu kulipa sh 700,000.


source: mpekuz

Read More »

Join Swahili One Community, "Like" and you will be one of us forever

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Copyright © 2013. swahili one Blog - All Rights Reserved
Customized by: Grace Tommy The One | Powered by: BS
Designed by: Creative Blogger