Showing posts with label Magazeti na Picha. Show all posts

Mwanzo Mpya Kwa Feza Kessy Baada ya Oneza Kufungasha Virago BBA The Chase.


Katika Eviction ya wiki hii tumeshuhudia shemejiii yetu Oneal akiyaaga mashindano yao huku akimwacha mkewe, Mshiriki na mwakilishi aliyebaki mjengoni humo baada ya Nando kuondolewa kwa sababu za kiusalama.

Ingawa Feza amekuwa disappointment machoni kwa mashabiki wengi wa Tanzania kutokana na kusahau kilichompeleka huko, naimani hii itakuwa fursa ya kipekee kwake kujipanga na kurudisha akili yake katika Shindano Hilo.

Mshiriki Nando ambaye alienguliwa katika shindano hilo ndo alikuwa anapewa nafasi kubwa ya ushindi, nna uhakika kilichomkuta kitakuwa fundisho kwa wawakilishi watarajiwa katika Mashindano yajayo.

Read More »

Machangu wajiuza karibu na nyumba ya Waziri Mkuu







--> KWELI ni aibu kwa taifa kama la Tanzania, lenye ulinzi uliotimia lakini ni ajabu sana kuwaona wanawake wanaoishi mjini kwa kutegemea biashara haramu ya kuuza miili ‘machangudoa’ wamefikia kuifanya jirani kabisa na makazi ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Mizengo Pinda.

WANASWA NA MAPAPARAZI
Wiki iliyopita, mapaparazi wetu  waliwanasa machangudoa hao wakiwa wanazurura kwenye Barabara ya Kenyatta inayopita mbele ya makazi ya waziri mkuu takriban mita 80 kutoka barabarani kwa lengo la kujiuza.
Ili kulijua hilo kwa undani, mapaparazi wetu walijifanya wateja kabla ya kuwapiga picha ili kuweza kuzungumza nao mawili matatu kuhusu kuwepo eneo hilo lenye heshima zake.
Mmoja wa ‘wauza sukari’ hao aliyejitambulisha kwa jina la Hawa, mkazi wa Kinondoni, alikiri yeye na wenzake kufanya biashara hiyo kwenye eneo hilo.
“Ni kweli mimi na wenzangu tunapiga kambi eneo hili, huwa ikifika usiku tunaanzia kule Coco halafu tunakuja hadi huku, lakini mbona maswali mengi, unataka tufanye biashara kama vipi sepa,” alisema changu huyo akianza kupandisha jazba.

WATEJA WAO WAKUBWA NI HAWA
Kikubwa walichokiongea machangu hao walisema barabara hiyo yote hupitwa na viongozi wakubwa na wafanyabishara ambao baadhi yao ni wateja wao wakubwa. Wakasema hawamwamini sana mteja anayekwenda na Bajaj au Bodaboda kwa vile wanasumbua kutafuta eneo la kufanyia ngono.
“Wateja wetu wengi ni wale tunaomalizana ndani ya gari, hawa wa Bajaj na Bodaboda wengi wanataka kwenye majani, ni rahisi kukamatwa na polisi wa doria,” alisema changudoa mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Suzy lakini hakuwa tayari kutaja yaliko makazi yake.

CHAKUJIULIZA SASA
Inakuwaje wauza miili hao watanue eneo ambalo kimazingira linapitiwa na viongozi mbalimbali wazito kama vile mabalozi wa nje waliopo Tanzania, mawaziri, akiwemo waziri mkuu mwenyewe ambaye ni jirani kabisa na makazi yake?

ASKARI WAPO WAPI?
Yapo madai kwamba, askari wanaovalia mavazi ya kiraia ambao wanapaswa kuhakikisha usalama wa eneo lote la Coco Beach wanakaushia matendo hayo kwa kile kinachodaiwa wanapozwa na kitu kidogo.
“Askari wapo, lakini sema baadhi yao wanatufahamu, kwa hiyo ikitokea na sisi mambo yetu yamekaa vizuri tunachekiana,” alisema Suzy.


Source:gpl

Read More »

Mama aliyemtesa mtoto ahukumiwa

HATIMAYE haki imetendeka, hayo ni maneno waliyoyasema baadhi ya wakazi wa Mbeya waliohudhuria katika Mahakama ya Wilaya na kushuhudia Wilvina Mkandara (24) akihukumiwa kifungo cha maisha jela kutokana na kesi iliyokuwa inamkabili ya kumtesa hadi kumsababishia ulemavu mtoto, Aneth Johannes (4) aliyekuwa akimlea.


--> Mara baada ya hukumu hiyo kutolewa Jumatatu iliyopita na hakimu mkazi aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo, Gilbert Ndeuruo, wananchi walionekana kufurahi na wengi wakitaka japo kumgusa mfungwa huyo mpya lakini ulinzi wa polisi ulikuwa imara.
“Huyu mama angenyongwa tu,” alisikika akisema mama mmoja aliyeonesha kuwa na hasira na mfungwa huyo aliyekuwa amezungukwa na askari polisi.

Akisoma hukumu hiyo iliyozusha cherekochereko kutoka kwa baadhi ya wakazi hao wa Mbeya mahakamani hapo, Hakimu Ndeuruo alisema mshitakiwa amehukumiwa kutokana na kifungu cha 235 cha mwenendo wa makosa ya jinai cha mwaka 1985.

Akaongeza kuwa mahakama hiyo imeona mshtakiwa anastahili adhabu kutokana na mtuhumiwa huyo kama mzazi kushindwa kujali afya ya mtoto wakati alikuwa mama mlezi ikiwa ni pamoja na kumpeleka hospitali kwa wakati ili apatiwe matibabu.

Hakimu Ndeuruo amesema mahakama hiyo haikuridhishwa na ushahidi wa utetezi wa mtuhumiwa alioutoa mahakamani kuwa majeraha yaliyokutwa mwilini mwa mtoto Aneth yalitokana na kuugua tetekuwanga, jambo ambalo alisema si la kweli.

Aidha, mshtakiwa Wilvina alipotakiwa kujitetea ili apunguziwe adhabu kabla ya kusomewa hukumu alisema: “Naiomba mahakama inipunguzie adhabu kwa kuwa mimi ni mjamzito pia sijui mwanangu niliyemzaa alipo kwani sina mawasiliano na familia yangu.”

Akitoa hukumu hiyo Hakimu Ndauruo alisema amesikitishwa na kitendo cha mtuhumiwa huyo kutotaka kujua alipo mtoto aliyemkosea na badala yake kumjali wake. Mwanamke huyo alipandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza Novemba 16, mwaka jana.

Read More »

Join Swahili One Community, "Like" and you will be one of us forever

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Copyright © 2013. swahili one Blog - All Rights Reserved
Customized by: Grace Tommy The One | Powered by: BS
Designed by: Creative Blogger