Kizimbani kwa kosa la "KUMKABA" mwenza wake!!

Akitoka mahakamani

Blaithin Crombie, 49 aliyewahi kuwa mshauri wa masuala ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ambaye kwa sasa anajishughulisha na masuala ya Urembo, amepandishwa kizimbani baada ya kufunguliwa mashtaka na Aliyekuwa mpenzi wake (ambaye ni mwanasheria) kwa tuhuma za kumkaba na kumsababishia maumivu na msuguano katika ngozi ya koo.

Mtuhumiwa huyo anadaiwa kulifanya kosa hilo usiku wa majuzi ambapo alimwalika mwanasheria huyo kwa ajili ya kinywaji mida ya usiku, na pindi mwanaume huyo alipohitaji kuondoka, mwanamke huyo alisimama mlangoni na kumzuia asiondoke (kuna kitu alikuwa anahitaji...!!), baada ya kushindwa kumshawishi ndipo alipoaamua kumkaba koo kuashiria hasira zake.

Kwa mujibu wa sheria za Marekani, Blaithin crombie anaweza akaenda jela mwaka mzima kwa kosa la udhalilishaji wa kijinsia.

Join Swahili One Community, "Like" and you will be one of us forever

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Copyright © 2013. swahili one Blog - All Rights Reserved
Customized by: Grace Tommy The One | Powered by: BS
Designed by: Creative Blogger