Rais Barack Obama Atimiza Miaka 52, Bila Kuzima japo Mshumaa mmoja Hadharani.
Rais wa Marekani Barack Obama Ametimiza Miaka 52 Jumapili ya Jana.Hakukuwa na Sherehe Rasmi za kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa kiongozi huyo zaidi ya kuonekana siku ya Jumamosi akicheza Golf na Rafiki zake huko Camp David.
Ikulu ya Marekani haikusema ni vipi Amiri Jeshi huyo amesherehekea siku hiyo muhimu kwake. Alirudi majira ya Saa 8 Mchana Akiwa na Marine One, Akaingia ndani. Wakati akikaribia kuingia ndani ilisikika sauti kubwa ikisema "HAPPY BIRTHDAY" kutoka kwa mmoja wa wananchi aliyejitokeza kushuhudia kama kutakuwa na lolote.
Kiongozi huyo aligeuka, akatabasamu kisha akawapungia mkono. Hapakuwa na dalili za sherehe tena.