Salamu ya Heshima Toka kwa Rais Banda kwenda kwa Rais Kikwete
Katika Jambo Ambalo Mwanamke huyu analizingatia ni Mila za Heshima za Kwao, Ijapokuwa ki Utawala wana nafasi sawa na Rais Jakaya Kikwete, lakini Rais huyu wa Malawi aliweza kumpigia Magoti na kutembea mpaka alipo Kikwete Kumsalimia.
Mwanamama huyu machachari aliwahi kutajwa na Forbes kuwa anashikilia nafasi ya 71 Dunia katika orodha ya Wanawake Majasiri Mnamo mwaka 2012 na akapanda hadi nafasi ya 41 Mnamo mwaka 2013.