Mtanzania wa Miaka 14 Aibuka Bingwa wa Kuruka Kamba Duniani, Ampa Faraja Rais Kikwete.

-->

 Rais Kikwete akiwa na bingwa wa dunia Hamisi Mohamed pamoja na wachezaji wenzie na viongozi wa timu ya Tanzania iliyoshiriki katika mashindano ya dunia 
 Bingwa wa dunia wa kuruka kamba akionesha medali na kombe alivyonyakua Marekani
 Hamisi Mohamed na wenzake wakionesha umahiri wao wa mchezo wa kuruka kamba ambao unazidi kupata umaarufu duniani kote
 Hamisi akionesha manjonjo yake Ikulu
 Rais Kikwete akiangalia medali kibao alizoshinda Hamisi Mohamed.
Rais Kikwete akimpongeza kijana Hamisi kwa kutwaa ubingwa wa dunia na kuipatia sifa Tanzania ambayo kwa miaka mingi haijashinda medali yoyote katika michezo ya kimataifa.
Mwenyekiti wa Sport  Training Centre (TSTF), Dennis Makoi
amesema  kuwa walipotambua kuwa kijana
huyo anakipaji cha mchezo huo waliamua kumtafutia mfadhili ili kukiendeleza. 
Alisema kuwa walipata mfadhili kutoka Marekani ambaye anamiliki
kituo cha kufundishia mchezo huo ambaye alimchukua Hamisi kwenda Marekani
Desemba mwaka jana kwa ajili ya kuendeleza mafunzo hayo.
Makoi alisema kijana huyo akiwa katika kituo cha mfadhili
huyo  alishiriki mashindano ya dunia ya mchezo wa kuruka kamba yaliyofanyika
Julai 5 hadi 13 mwaka huu jijini Orlando, Marekani, yaliyokuwa na washiriki 480
kutoka  timu 44 kutoka nchi 14 ambapo
jumla ya wachezaji 6 walishiriki kutoka Tanzania na hatimaye kijana huyo
alinyakuwa kombe hilo na kuwa bingwa wa Dunia.
Amy Canady ambaye ni mfadhili wa kijana huyo alisema kuwa
amefurahishwa na jitihada za kijana huyo ambapo anafaa kuigwa na kupewa
usimamizi mkubwa, na kwamba lengo lao ni kujenga kituo cha mchezo huo Tanzania
ili kuukuza  ambapo vijana watapata fursa ya kucheza wakiwa nchini
kwao  na kuitangaza Tanzania.
Hamisi Mohamed alisema anashukuru kwa malezi aliyoyapata katika
kituo hicho cha watoto yatima cha Dogodgo Centre na kwa msaada waliojitolea
katika kukiendeleza kipaji chake.


Join Swahili One Community, "Like" and you will be one of us forever

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Copyright © 2013. swahili one Blog - All Rights Reserved
Customized by: Grace Tommy The One | Powered by: BS
Designed by: Creative Blogger