Criss Brown kwenda jela miaka 2
Taarifa kutoka Mtandao wa MTO zinasema msanii Criss Brown huenda akaenda jela miaka miwili na hukumu rasmi kutolewa Jumatatu ya leo.
Taarifa kutoka chanzo kinachoaaminikia na mtandao huo kimesema kuwa uamuzi umeshafikiwa na hukumu imeshaamuliwa, kilichobaki ni kumalizia taratibu za mwisho tu za tukio hilo. Si mwanasheria wa Criss au yeye mwenyewe anaweza kuzuia hukumu hiyo, labda Jaji abadilishe uamuzi wake, kitu ambacho hakitarajiwi.