Ndoa ya Will Smith Mashakani, picha za nyumba ndogo zanaswa.
Ndoa iliyodumu kwa zaidi ya miaka 16 kati ya msanii Will Smith na Jada Pinkett inaanza kusikia harufu ya talaka. Hayo yamekuja baada ya kuvuja kwa picha ambazo zinaonesha mwanaume akiwa katika ma pozi ya kimahaba na nyota Margot Robbie. Angalia Picho hapo chini ili nawe upate picha ya jinsi hali ilivyo.
Imeelezwa kuwa wawili hao waliondoka na kupotelea kusiko julikana kwa usiku mzima baada ya kumaliza mazoezi ya kazi ya filamu iliyokuwa mbele yao, hata hivyo kabla hawajaenda kujificha walionekana wakiwa katika hali ya kimahaba kwani walikuwa wakicheka kwa sauti na kukombatiana mara kwa mara kama vile wafanyavyo wapenz! wapya.