Nay wa Mitego ana Historia ya Kumpiga Baba yake Mzazi
Nay wa Mitego ni moja kati ya wasanii wenye tungo zenye utata sana tangu anaanza kufanya muziki ambapo alikuwa akisikika kwenye baadhi ya ngoma akimchana hata baba yake mzazi kwa kushindwa kuwa responsible kwake.
Hit maker wa ‘Muziki Gani’ ambae anakiri kuwa zamani alikuwa mkorofi sana na kwamba sasa hivi amebaki kuongea tu kwenye muziki, amewahi kufunguka kuwa alimpa kichapo baba yake wa kambo/baba yake wa kufikia ambae alikuwa akimtunza kwa muda huo.
Kisa cha kumpa kichapo mzee wa watu.. ni kwa sababu alikuwa anampiga sana mama yake Nay wa Mitego kitu ambacho kilikua kinamuumiza sana yeye, na mwisho wa siku akachukua uamuzi wa kumpiga akimtetea mama yake.
Tukio hilo lilimsukuma Nay wa Mitego kuandika mashairi ya wimbo unaohusu wanawake akiwaambia wanaume wenye tabia kama za baba yake wa kufikia kwamba ‘Mwanamke hapigwi, anatulizwa na mapenzi.’
“Ule wimbo ulikuwa ni dedication kwa mama yangu mzazi, mama yangu mzazi alikuwa anaishi na baba yangu wa kufikia, yule baba yangu alikuwa mkorofi sana, alikuwa anampiga sana mama bila sababu, kiasi kwamba alisababisha mimi na mama tusielewane kwa sababu mimi nilikua sipendi vile alivyokuwa anamfanyia mama, mi nakumbuka kwa bahati mbaya nilishawahi kumpiga yule mzee and then mama yangu akachukua hatua ambayo mimi sikuitegemea kwa sababu mimi nilikuwa namtetea mama.
“Mi nikajifunza kwamba mwanamke hatakiwi kupigwa hata siku moja, na ndo maana nikaimba, so ilikuwa dedication kwa mama yangu na wanawake wote Afrika.” Alisema Nay wa Mitego.