50 Cent Kwenda Jela Miaka 5 kwa Kosa la Kumshambulia Mpenzi wake na Uharibifu wa Mali.
Rapper na Muigizaji 50 Cent Amekana Mashtaka yanayomkabali ya Kumjeruhi na Kuvunja mali za aliyekuwa Mpenzi wake Dapne Narvaez. 50 Cent ambaye Jina Lake Kamili ni Curtis Jackson Alisimamishwa Kizimbani katika mahakama ya Van Nuys, California Jumatatu Asubuhi.
Ikiwa mahakama itampata na hatia kwa makosa hayo, Mwimbaji huyo wa In Da Club atatakiwa kutumikia Kifungo cha Miaka Mitano Jela na Kulipa Faini ya Dola za Kimarekani 46,000.
50 Akiwa Mahakamani Jana Asubuhi.
Kutokana na Mwenendo wa Kesi za Mashambulio kama hiyo, 50 Cent anatakiwa Asimkaribie Anaye Mshtaki kwa Futi 100, wala kuwasiliana nae au familia yake kwa kipindi chote ambacho kesi itakuwa Ikiunguruma. Mbali na hayo Curtis ameambiwa asalimishe Bastola yake na Silaha nyingine anazomiliki ndani ya Masaa 24.
Daphne anamshtaki 50 Cent kwa kumvamia nyumbani kwake, kumpiga na kusababisha uharibifu wa mali zenye thamani ya Dola za Kimarekani 7,000.