Mrembo aachwa na Mpenzi wake baada ya kuweka picha hii Face Book.
Siku chache zilizopita imeshuhudiwa kuvunjika kwa uhusiano wa muda mrefu baina ya msichana aneyeonekana katika picha na Mchumba wake kutokana na kukasirishwa kwa mwanaume huyo na kitendo cha Msichana huyo kuiweka picha hiyo Face Book.
Katika kuelezea kilio chake katika Ukurasa wake huo, binti alielezea ni jinsi gani anapenda kujipiga picha kiasi cha kufikia kununua Camera ya gharama huku akielewa ya kwamba mwanaume huyo analifahamu hilo na ndio maana hakusita kujipiga picha za aina hiyo na kuzitupia mtandaoni.
Alihoji ya kwamba iwapo kuna mapenzi ya kweli basi picha hiyo si ya kuvunja uhusiano wao!!! Vipi wewe unalionaje hili?