Mahakama yamuachia Huru George Zimmerman, Muuaji wa Mmerakani mweusi Trayvon Martin
Mahakama imemuachia huru George Zimmerman, 29, na mashataka ya mauaji yaliyokuwa yanamkabili. George alikuwa na kesi ya kumua Trayvon Martin,17 Mmarekani mweusi kwa kumpiga Risasi na kumuua mnamo mwezi wa pili 2012. Baada ya mwaka na miezi ya kuunguruma kesi hiyo, mahakama imeona mauaji hayo hayakuwa ya kukusudia. Ingawa George ameachiwa huru maisha yake yapo hatarini sana kwani wengi wa watu weusi waishio Marekani wametafsiri suala hilo kama ni la kibaguzi na kwamba kwa kuwa aliyeuliwa ni mtu mweusi ndo maana ameachiwa huru.
Miongoni mwa watu waliolalamika ni Msanii Akon ambaye katika Twitter page yake amesema kuwaambia Watu weusi ya kwamba Marekani si nchi yao, waondoke warudi Africa ambapo watahudumiwa kama wafalme bila utabaka.