Polisi yawasaka Waliofanya Mapenzi katika treni
Polisi inaendelea na uchunguzi ili kuwabaini binadamu wawili waliokosa haya na kuamua kurekodi video yao ya mapenzi ndani ya usafiri wa jumuiya, train. Video hiyo ambayo inaonekana ilirekodiwa kupitia simu ya mkononi, iliwekwa mtandaoni mara ya kwanza alhamisi iliyopita kupitia facebook lakini iliondolewa baadae, mpaka sasa imeshatazamwa mara Mil1.4.
Wasemaje wa kampuni hiyo ya usafirishaji wamesema ya kwamba kitendo hicho walichokifanya raia hao si kwamba tu hakipendezi bali ni kinyume na sheria, na endapo watakamatwa watazuiwa kutumia usafiri huo wa jumuiya kwa kipindi kisichopungua mwaka mmoja.