KHLOE KARDASHIAN AFUNGUA KESI YA MADAI YA TALAKA KWA LAMAR, NI BAADA YA MUMEWE HUYU KUZIDISHA USALITI


Inaonekana matatizo ya ndoa ya Khloe Kardashian kwa Lamar Odom yameshafika ukingoni, hii ni kutokana na kuwepo kwa taarifa kwamba nyota huyo wa vipindi halisia amefungua kesi ya madai ya talaka hapo jana.

Kardashian anategemea kutengana kimoja na mume wake ambaye ni nyota wa mpira wa kikapu, huku chanzo ikielezwa kuwa ni tofauti zao, TMZ imeripoti.
 
Wawili hao wametengana kwa kipindi cha miezi sasa, huku taarifa nyingine zikieleza kuwa Odom anahangaika juu ya ishu zake za madawa ya kulevya.

Nyota huyo wa vipindi halisia vya TV aliamua kumpiga chini Odom kimoja mara baada ya jamaa kuposti kwenye mitandao, video ya muziki wa rap iliyohusu usaliti, akisema: “Wakati Khloe akiwa nje ya mji, mimi naendelea kuwepo kwenye DL”.
 
Akiwa kwenye ndege kuelekea Australia Kardashian aliiona hiyo video ikiwa imeenea kwenye mitandao, na toka kipindi hicho Khloe hajawahi onekana akiwa amevaa pete yake ya ndoa.

DC Blog

Join Swahili One Community, "Like" and you will be one of us forever

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Copyright © 2013. swahili one Blog - All Rights Reserved
Customized by: Grace Tommy The One | Powered by: BS
Designed by: Creative Blogger