Gesti Bubu Nyingine Inayofuga Machangudoa Yabainika
MZEE mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Abdullahimu Mnami (48) amenaswa akiendesha gesti bubu kinyume cha sheria za nchi.
Baadhi ya wananchi walionaswa katika msako wa biashara haramu ya ukahaba. Pichani ni wauzaji na wanunuzi.
Tukio hilo lilitokea Oktoba 26, mwaka huu maeneo ya Tuangoma jijini Dar, baada ya waandishi wetu kuzinyaka taarifa hizo na kuzifikisha kwa mwenyekiti wa serikali ya mtaa huo, Chande Mohammed aliyefika eneo hilo na polisi.
Awali, ili kujiridhisha, mmoja wa mapaparazi wetu alijifanya mteja na kufika katika gesti bubu hiyo, kisha kupangisha chumba kwa malazi ya siku moja kwa malipo ya shilingi 3000 tu lakini pasipo kuandikisha mahali popote.
Akizungumza na waandishi wetu mbele ya maaskari na mwenyekiti, mzee huyo alisema alishindwa kuisajili gesti yake kwa kuwa haikuwa na viwango vinavyokubalika na manispaa (ya Temeke).
“Ningefuata utaratibu, manispaa isingeniruhusu kutokana na ubora wa vyumba vyenyewe, kama mnavyoona. Pia njaa tu jamani ndiyo imenifanya nianzishe gesti hii,” alisema mzee Abdullahim.
Hata hivyo mwenyekiti wa mtaa huo, alisema kuwa mzee huyo ana kesi ya kujibu kwa kukiuka taratibu za kibiashara zilizowekwa na halmashauri na kumuamuru aifunge gesti hiyo mara moja huku akiahidi kumpeleka Baraza la Kata kwa ajili ya masikilizano ya awali.
Timu yetu iliwaachia msala wao na kuendelea na oparesheni nyingine ambapo walifanikiwa kuwanasa machungudoa wakijiuza jirani na mtaa huo huku ikielezwa kuwa, wateja wa madadapoa hao hupelekwa katika gesti bubu ya mzee huyo kwa vile ni bei poa.
GPL
Posted by
Unknown

Related Articles
- HEMED 'PHD' ALA SHAVU LA KUIGIZA FILAMU ZAMBIA.
- ABAKWA, ANYONGWA HADI KUFA NA KISHA KUINGIZWA CHUPA SEHEMU ZA SIRI HUKO CHALINZE
- MACHANGU NA WATEJA WAO WAKAMATWA NA OFM YA MWISHO MWAKA, BALAA.
- BAADA YA KUKAA KAMA WACHUMBA KWA MIAKA 15, MAMA TUNDA ATEMANA NA AFANDE SELE.
- CHUCHU HANS AJICHORA TATOO YA RAY, NI KUONESHA JINSI GANI MAHABA YAO YAPO JUU
- WEMA AWATIBUA FANS WAKE NA VIVAZI VYAKE VYA UTATA
- ANAETAKA KUMWOA LULU KUTOA MAHARI YA TSH LAKI 8
- Lina asaka Mimba
- NAY WA MITEGO ABAMBWA AKIWA NA LUNDO LA MABINTI, MANAIKI STYLE.