BRUNO MARS NDIO MWANAMUZIKI BORA WA BILLBOARD 2013


Huenda Miley Cyrus ameongoza zaidi kwa kuwa juu nabni ukweli usiopingika kwamba Justin Timberlake amerudi kwa kishindo kwenye muziki, ila habari sahihi ni kwamba Bruno Mars ndiye ambaye ametajwa kuwa msanii bora wa Billboard kwa mwaka 2013.
"Ni maendeleo, ni heshima," Mars alisema kwenye mahojiano wiki hii. "Najisikia fahari kuwa sehemu ya timu hii yote niliyonayo."

Nyimbo za mwaka huu za mwimbaji huyo zinahusisha pia wimbo namba moja When I Was Your Man na ngoma namba 5 akiwa na Treasure.

Album yake kali, Unorthdox Juxebox, ilizinduliwa mwaka jana na imeuza zaidi ya nakala 1.8 million. Ikiwa ndiyo album ya pili bora kimauzo nyuma ya album ya Timberlake iitwayo The 20/20 Experience.

Join Swahili One Community, "Like" and you will be one of us forever

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Copyright © 2013. swahili one Blog - All Rights Reserved
Customized by: Grace Tommy The One | Powered by: BS
Designed by: Creative Blogger