CHUCHU HANS AJICHORA TATOO YA RAY, NI KUONESHA JINSI GANI MAHABA YAO YAPO JUU


KATIKA hali inayoonesha kuna kitu kikubwa kinakuja mbeleni, msanii wa filamu, Chuchu Hans amejichora ‘tatuu’ inayosomeka kwa jina la Ray huku anayedaiwa kuwa mpenzi wake, Vincent Kigosi ‘Ray’ naye akiwa amejichora tatuu inayosomeka kwa jina la Chuchu.
Ray na Chuchu.
Picha ambazo gazeti hili limezinasa zinawaonesha wawili hao wakipigia ‘promo’ uhusiano wao huku wadau wengi wakiyafananisha mapenzi yao na ya njiwa.
Ili kujua undani juu ya jambo hilo, mwandishi wetu aliwatafuta wasanii hao ambapo Chuchu alionekana kukerwa na swali hilo na kujibu kwa ufupi kuwa hataki kusumbuliwa.
“Hivi hamchoki kufuatilia maisha ya watu jamani? Naomba mniache,” alisema Chuchu Hans.



Kwa upande wa Ray, simu yake ya mkononi iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa.

GPL

Join Swahili One Community, "Like" and you will be one of us forever

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Copyright © 2013. swahili one Blog - All Rights Reserved
Customized by: Grace Tommy The One | Powered by: BS
Designed by: Creative Blogger