WEMA AWATIBUA FANS WAKE NA VIVAZI VYAKE VYA UTATA



BEAUTIFUL Onyinye, Wema Sepetu ameendelea ‘kutibua’ hali ya hewa kwa kukiuka maadili ambapo kwa mara nyingine tena ametupia picha mtandaoni zikimuonesha akiwa amevaa mavazi yaliyoacha wazi baadhi ya sehemu nyeti za mwili wake.
Wema Sepetu.
Picha hiyo iliyopo kwenye baadhi ya mitandao ya kijamii inamuonesha Wema akiwa amevaa kiblauzi chenye matundu kiasi cha kuifanya sidiria aliyovaa ionekane huku sehemu nyingine zikiwa wazi.
Wakiizungumzia picha hiyo ambayo Wema anaonekana akiwa na rafiki yake, Kajala Masanja, baadhi ya wadau wamesema msanii huyo anaonekana kujisikia raha sana sehemu zake kuwa wazi.



“Mh! Huyu Wema na hivi vivazi vyake vya nusu utupu hajambo, sijui anajisikiaje kuvaa vile…hata kama atasema ni kutokana na hali ya joto lakini hii sasa imezidi, huko ni kuwatega wanaume,” aliandika mdau mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Mwanaidi.


GPL

Join Swahili One Community, "Like" and you will be one of us forever

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Copyright © 2013. swahili one Blog - All Rights Reserved
Customized by: Grace Tommy The One | Powered by: BS
Designed by: Creative Blogger