Diamond na Davido ndani ya remix ya " My number one "
Davido na Diamond wameamua kuingia studio na kufanya remix ya wimbo wa My number one wa msanii Diamond.
Wimbo huo wali-perform kwa mara ya kwanza kwenye show ya fiesta iliyofanyika jana kwenye viwanja vya Leaders club.Bado taarifa za uwezekano wa wawili hao kufanyia video ya wimbo huo hazijatoka..
Show ya pamoja kati ya Diamond na Davido ilikuja baada ya show kali aliyofanya Davido ambayo ilivutia wapenzi wengi wa muziki waliofika kwenye uwanja wa Leaders kwa ajili ya kuangalia performance za wasanii ambao hawakuweza kupanda usiku wa Jumamosi.