Mwanafunzi Akutwa Amekufa Huku Akiwa "UCHI" chumbani kwake.
-->
Mwanafunzi kutoka Ebony State University, Aliyefahamika kwa jina la Miracle Eze amefariki dunia huku akiwa hana nguo hata moja (uchi) ndani ya chumba chake katika Campus ya Iseheke Chuoni hapo.
Miracle Enzi za Uhai wake |
Mwanafunzi kutoka Ebony State University, Aliyefahamika kwa jina la Miracle Eze amefariki dunia huku akiwa hana nguo hata moja (uchi) ndani ya chumba chake katika Campus ya Iseheke Chuoni hapo.
Siku moja kabla ya kufikwa na umauti, Miracle alienda chumbani kwa rafiki yake huku akilia machozi na kumweleza ni jinsi gani kuna mtu anamtishia maisha sababu ya kutomkubali kama mpenzi wake na anahisi atamfanyia kitu kibaya kama alivyomuahidi.
Asubuhi yake wenzake walipopita mlangoni kwake na kugonga hawakujibiwa, kwa kuwa walikuwa na haraka ya kuwahi masomo walihisi atakuwa anasali chumbani humo, lakini hadi wanatoka darasani binti huyo alikuwa hajaonekana na ndipo walipoamua kumpigia simu yake ya kiganjani ambayo ilikuwa inaita tu bila majibu.
Walisogea mlangoni na kuisikia simu ikiita, baadhi ya wavulana waliamua kupanda kwa dirishani kuchungulia ndani na ndipo walipomuona akiwa katika hali hiyo, taarifa zikatolewa Polisi ambao walifika na kuuchukua mwili huo huku Juhudi za kubaini chanzo cha kifo chake zikianza.