Brad anunuliwa Kisiwa chenye umbo la Kopa na Jolie kama zawadi ya Miaka 50 ya Kuzaliwa
Ni kitu gani unachoweza kumpa mtu ambaye anakaribia kuwa na kila kitu? Kisiwa...!
Kwa mujibu wa taarifa mpya, Angelina Jolie ametenga kiasi cha $19million kwa ajili ya kunua kisiwa chenye umbo la moyo ambacho kipo kwenye Ziwa Mahopac, maili 50 toka jiji la New York City, kisiwa ambacho imetaarifiwa kwamba ana mpango wa kumpa mpenzi wake Brad Pitt kama zawadi kwa kutimiza miaka 50 hapo itakapofika December 18.
Hivi karibuni Angelina alitembelea kisiwa cha Petra ambapo alikuja kugundua kwamba kulikuwa na mijengo miwili ya hatari ambayo ilisanifiwa na Frank Lloyd Wright, ambaye ndiye msanifu namba moja apendwaye na Brad. Inaelezwa kwamba aliweza kununua moja kati ya mali hizo.
"Mara baada ya kusikia kisiwa hicho kipo sokoni Angelina alipanga kwenda kukiona, hakika alivutiwa sana. Nyumba ipo kwenye mazingira mazuri ya wawili kuishi au hata kwa ajili ya familia," chanzo kimoja kiliieleza Daily Mirror U.K.
"Kipo kibinafsi na Angelina anafahamu ukweli kwamba kisiwa hicho kina umbo kama la moyo kitu ambacho kitamaanisha sana kwa jamaa," chanzo kilifafanua.