BAADA YA KUKAA KAMA WACHUMBA KWA MIAKA 15, MAMA TUNDA ATEMANA NA AFANDE SELE.
KUCHA za Shetani zimeugusa uchumba wa muda mrefu kati ya msanii Selemani Msindi ‘Afande Sele’ na Asha Shiengo ‘Mama Tunda’ ambapo inadaiwa sasa kila mmoja yuko na ‘hamsini’ zake, Ijumaa linaibumburua.
Picha ya familia: Kutoka kulia ni Asha Shiengo ‘Mama Tunda’, Selemani Msindi ‘Afande Sele’, Asantesana Selemani na Tunda Selemani.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, kutoelewana kwao kunachangiwa na kucheleweshwa kwa ndoa baina yao pamoja na mambo mengine ambayo hakuwa tayari kuyaanika.
“Kwa kifupi mapenzi sasa hivi kati ya Afande na Mama Tunda ni ‘vululuvululu’, kila mmoja yuko kivyake.
“Chanzo kikubwa ni kucheleweshwa kwa ndoa ambapo Afande anaonekana kupotezea suala la kuoana ,” kilisema chanzo hicho kwa sharti la kutotajwa jina lake gazetini.
“Chanzo kikubwa ni kucheleweshwa kwa ndoa ambapo Afande anaonekana kupotezea suala la kuoana ,” kilisema chanzo hicho kwa sharti la kutotajwa jina lake gazetini.
Mwandishi wetu alipomtafuta Afande Sele kuweka wazi juu ya tuhuma hizo, kwa sauti ya upole kabisa alikiri kutokuwepo maelewano baina yake na mzazi mwenziye huyo huku akishindwa kubainisha haswa chanzo cha kutengana kwao.
“Ni kweli, kwa sasa siko na Mama Tunda, mimi niko Morogoro na yeye yuko Dar,” alisema msanii huyo bila ufafanuzi wa ziada.
Hata hivyo Mama Tunda alipotafutwa kwa njia ya simu, alissema chanzo cha mambo yote ni kutovalishwa pete ya ndoa.
Hata hivyo Mama Tunda alipotafutwa kwa njia ya simu, alissema chanzo cha mambo yote ni kutovalishwa pete ya ndoa.
“Chanzo ni hicho tu, nimechoka kukaa kwenye uchumba kwa muda mrefu ni miaka 15 sasa, hadi Tunda amefikisha miaka 13, si ni ajabu hiyo na sasa tuna mtoto wa pili ambaye ana miaka 2 bado ni wachumba tu, nimechoka,” alisema Mama Tunda na kisha kukata simu.
GPL