Wazichapa Hadharani wakigombania Ulabu



AMA kweli duniani kuna vitimbi! Huwezi amini, wanaume wawili waliotajwa kwa jina mojamoja, Ndalo (45) na Songoro (62) wamenaswa wakizichapa kavukavu kabla ya kutumbukizana kwenye kinyesi wakigombea pombe ya kienyeji.

Tukio hilo la aina yake lilijiri hivi karibuni Maeneo ya Stendi ya Mabatini jijini hapa ambapo kwa mujibu wa mashuhuda wa sinema hiyo ya bure, wawili hao walipewa ofa ya pombe ya kienyeji aina ya kindi na rafiki yao aliyeondoka mapema eneo hilo.

Mashuhuda hao walitiririka kuwa kabla ya kuanza kuinywa pombe hiyo ambayo hunywewa kwa kupokezana kwenye kikombe kikubwa (koronto), Ndalo aliitwa na mteja kuelekea kwenye kibanda chake kumhudumia ambapo inadaiwa kuwa alitumia muda mrefu huko wakati Songoro akikamata fursa kwa kuigida pombe yote bila kubakisha hata tone.

Ilielezwa kuwa baada ya kurudi na kukuta pombe yote imeisha, Ndalo alianzisha timbwili kiasi cha kushikana mashati na Songoro ambaye muda huo alikuwa chakari kutokana na pombe hiyo ya ofa.

Wawili hao walizichapa kavukavu na kutumbukia kwenye tope la mtaro wenye kinyesi huku Songoro akionekana kuzidiwa nguvu na kukandamizwa almanusura apoteze uhai.

Hata hivyo, wawili hao walitenganishwa na wasamaria wema.

GPL

Join Swahili One Community, "Like" and you will be one of us forever

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Copyright © 2013. swahili one Blog - All Rights Reserved
Customized by: Grace Tommy The One | Powered by: BS
Designed by: Creative Blogger