Rose Ndauka anamuamini Hubby aliompa ujauzito wake
STAA wa sinema za Bongo, Rose Ndauka amesema suala la kubeba mimba ya mpenzi wake, Malick Bandawe kabla ya ndoa halikutokea bila mpangilio, walishauriana kabla.
Akipiga stori na paparazi wetu, Rose alisema hajutii kubeba mimba hiyo ambayo ameitangaza kwa vile alishauriana na mwandani wake huyo na anamuamini.
“Sijajibebea tu mimba hovyohovyo hata Malick alipogundua hali hii alifurahi sana, ndiyo maana sina presha hata kidogo kwa kuwa sisi ni wapenzi wa muda mrefu na tunaaminiana,” alisema Rose.
GPL.