Dereva Aliyemgonga Askari na Kumuua Papo Hapo Kortini

DEREVA anayetuhumiwa kwa kesi ya kusababisha kifo cha askari wa usalama barabarani, Koplo Elikiza Nnko, Jackson Steven Simbo (pichani) amefikishwa mahakama ya Kinondoni, Dar, Machi 26,  mwaka huu na kuzua jambo kortini.
Mtuhumiwa huyo baada ya kupata dhamana alikwenda ofisini kwa maofisa wa mahakama hiyo na kubadili shati kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kuondoa nuksi ya kulala rumande kwa siku 8.
Jackson anakabiliwa na makosa matatu,   kusababisha kifo cha Koplo Elikiza, kuendesha gari kwa mwendo kasi na kuingilia msafara wa kiongozi na kushindwa kujisalimisha polisi hadi alipokamatwa. Kesi hiyo itatajwa tena Aprili 15, mwaka huu.

Source:gpl

Join Swahili One Community, "Like" and you will be one of us forever

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Copyright © 2013. swahili one Blog - All Rights Reserved
Customized by: Grace Tommy The One | Powered by: BS
Designed by: Creative Blogger