Aunt Lulu atangaza kuachana na biashara ya Ukahaba.....Awataka wateja wake waache kumtafuta kwa sasa
Msanii Lulu Mathias Semagongo ‘Anti Lulu’ ameibuka na kusema kuwa sasa hawezi kurudia biashara ya kujiuza na kuwataka wanaodhani kuwa bado yuko na tabia hiyo waondoe hisia hizo kwani kwa sasa si Lulu wa zamani tena.
Akizungumza na mwandishi wetu, Anti Lulu alisema sasa hivi amejipanga kuyaendesha maisha yake kihalali na kwa kiasi kikubwa amefanikiwa licha ya kuwepo kwa baadhi ya watu wanaotaka kumrudisha nyuma.
“Watu wameniibia dukani kwangu ili kunirudisha nyuma lakini hawaniwezi, siwezi kuurudia ukahaba tena.
"Nilikuwa najiuza kutokana na hali ngumu ya maisha. Kwa sasa maisha yangu yamenyooka na sioni haja ya kuitwa kahaba tena.
"Nataka wanaume wanaodhani bado najiuza waelewe hivyo.Mimi ni Lulu mpya.Nimeshanunua uwanja Bunju na muda si mrefu ntaanza kujenga"..Aunt Lulu