Pombe zilinifanya Nimbusu Harrysong, Ajitetea Mrembo.
Muigizaji wa nollywood asiyeishiwa Scandals, Uche Ogbodo, amejitetea baada ya kuvuja picha zikimwonesha anambusu mume wa mtu, msanii wa muziki, Rapper Harry Song. Katika kujitetea huku alisema ya kwamba yeye na Harry ni watu wa karibu na marafiki wa kawaida tu wa muda mrefu.
"Hakuna jingine kati yetu, na hilo busu lilikuwa la kirafiki tu kwani siku hiyo ilikuwa Birthday ya Harry, hivyo tuli kiss kama kuonesha furaha ya siku hiyo" Alisema Uche.