Chup! ya kike, Sidir!a na kifulana cha kike vyadaiwa kuivunja ndoa ya Bob Junior
Ndoa ya mwanamuziki wa bongo flava, Raheem Nanji 'Bob Junior' na kinara wa filamu ya laptop, Halima Ali 'Ritha' imebainika kwenda mrama kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ni muigizaji wa filamu za kiswahili wa Kenya, Ashuu Daniel 'Ashley Toto' mwenye makazi yake nchini ujerumani.
Kwa mujibu wa habari ambazo mwandishi wetu amezipata, Ashley ambaye pia ni promota anayefanya kazi na wanamuziki wa afrika mashariki kwa kuwandalia maonesho nchini ujerumani, amekuwa akitajwa sana na mke wa Bob Junior kuwa ameingilia kati ndoa yake kwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mumewe.
Mgogoro huo ulikuwa ukisababisha migongano ya mara kwa mara kati ya wanandoa hao kiasi cha kujikuta wakigombana mara kwa mara karibu kila siku na hasa inapotokea Bob Junior kuwasiliana kwa simu na Ashley kwa mazungumzo ambayo yalikuwa na ashirio la kubemelezana kimapenzi baina yao.
Aidha, hivi karibuni mgogoro wa wanandoa hao ulikolea zaidi baada ya Bob Junior kurejea kutoka Kenya alikokuwa na Ashley ambaye kwa sasa yupo mapumzikonu nchini kenya, ambapo baada ya kupekuliwa kwenye begi lake na mkewe alikutwa na chupi ya kike, sidiria na kifulana cha kike.
''Bob Junior alikuwa ametoka Kenya na akawa akijiandaa kwenda Mbeya kwenye shoo nyingine, sasa mkewe akawa anamuandalia nguo zake kwaajili ya safari ya Mbeya.... Sasa katika kupekua pekua, ndio akakutana na sidiria na chupi ya kike ambazo zilishavaliwa bila ya kufuliwa'' kilisema chanzo kimoja cha habari hii.
Imeelezwa, migogoro ulikolea zaidi kutokana na kifulana (top) kilichofumwa na kutambuliwa na mke wa Bob Junior kuwa ni cha Ashley kutokana na kuwahi kumuona amekivaa katika moja ya picha zake katika tovuti ya facebook..
Hali hiyo iliibua ugomvi mzito hadi mkewe akaamua kufunga mizigo yake na kurudi kwao Unguja.
Bob Junior na Ashley Toto
Aidha, mwandishi wetu alizungumza na mke wa mwanamuziki huyo na kukiri kutokea mgogoro baina yake na mumewe kiasi cha kuamua kurudi kwao Zanzibar kwa muda na kusubiri kikao cha upatanishi ambacho hajui kitafanyika lini.
''Nimerudi Zanzibar na mwanangu, nasubiri hicho kikao cha kupatanishwa ila nasikitika sana kwa mume wangu kushindwa hata kujua hali ya mtoto na anajua wazi kama anaumwa, nahangaika nae peke yangu.. Sikutegemea kama mume wangu anaweza kufanya ushenzi kama huu,'' alisema.
Hata hivyo mwanamuziki huyo alipoongea nasi alikataa kutoa ufafanuzi wowote, lakini hivi karibuni alikaririwa na mtandao mmoja akikana kuwa na mke kwa sasa.