"Mapenz! ni sawa na Sumu Maishani" Johari
SIKU chache baada ya kuingia katika mgogoro na msanii mwenzake, Chuchu Hans kwa madai ya kugombea penzi la Vincent Kigosi ‘Ray’, muigizaji Blandina Chagula ‘Johari’ amesema amegundua mapenzi yanaumiza na ni sumu mbaya maishani.
Akizungumza na mwandishi wetu mwishoni mwa wiki iliyopita katika moja ya mahojiano maalumu, Johari alisema mapenzi si kitu cha kuendekeza kwani ni hatari na ndiyo maana baadhi ya watu hufikia hatua ya kuchukua uamuzi mgumu wa kujiua.
“Mapenzi ni kitu kingine kabisa, sikuwahi kujua ni kwa nini baadhi ya watu hufikia hatua ya kukatisha maisha yao kisa mapenzi, hakika mapenzi ni sumu kali sana maishani usipojiongoza,” alisema Johari.