Madawa ya Kulevya yampeleka Mbunge wa Kinondoni,Iddi Azzan Polisi.
-->
KUFUATIA kutupiwa skendo za kuhusika na usafirishaji wa madawa ya kulevya nje ya nchi, Mbunge wa Kinondoni jijini Dar, Idd Azzan ametinga polisi Julai 29, mwaka huu na kuwataka wamchunguze kwa kina.
“Kikubwa Azzan amemwambia Kova kwamba anataka jeshi la polisi limchunguze na kisha liwaambie wananchi kama yeye anahusika na biashara hiyo au la,” kimesema chanzo chetu.
Baada ya kupata habari hizo, Risasi Mchanganyiko lilimpigia simu Azzan ambaye alikiri kufika polisi na kuwataka wamchunguze kwa kina.
Hivi karibuni Mbunge huyo alitajwa katika habari zilizosambazwa mtandaoni kwamba anahusika na biashara hiyo baada ya mfungwa mmoja wa gereza moja nchini Hong Kong kumtaja kwamba ndiye anayewatuma vijana nje ya nchi kupeleka madawa ya kulevya.
Hata hivyo, Mbunge huyo amekanusha taarifa hizo kwa kusema kuwa hausiki kwa njia moja ama nyingine na kutaka mfungwa huyo atajwe jina lake kamili, namba yake ya ufungwa na hata ndugu zake waliopo hapa nchini ili ukweli ujulikane.
Barua zilizosambazwa mtandaoni ambapo jina la Mhe. Idd Azzan lilitajwa kuhusika na dawa za kulevya:
Source:GPL
KUFUATIA kutupiwa skendo za kuhusika na usafirishaji wa madawa ya kulevya nje ya nchi, Mbunge wa Kinondoni jijini Dar, Idd Azzan ametinga polisi Julai 29, mwaka huu na kuwataka wamchunguze kwa kina.
Madawa ya kulevya.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, Idd Azzan alifika katika Kituo Kikuu cha Polisi Posta jijini Dar na kukutana na Kamanda wa Kanda Maalumu, Kamishna, Suleiman Kova.“Kikubwa Azzan amemwambia Kova kwamba anataka jeshi la polisi limchunguze na kisha liwaambie wananchi kama yeye anahusika na biashara hiyo au la,” kimesema chanzo chetu.
Baada ya kupata habari hizo, Risasi Mchanganyiko lilimpigia simu Azzan ambaye alikiri kufika polisi na kuwataka wamchunguze kwa kina.
Mbunge wa Kinondoni jijini Dar, Idd Azzan.
“Kila kinapofika kipindi kama hiki huwa kuna vuguvugu la uchaguzi, hivyo maneno kama haya husemwa ili kuharibiana sifa, nimewataka polisi wanichunguze na watakachokipata watoe taarifa kwa wananchi,” alisema.Hivi karibuni Mbunge huyo alitajwa katika habari zilizosambazwa mtandaoni kwamba anahusika na biashara hiyo baada ya mfungwa mmoja wa gereza moja nchini Hong Kong kumtaja kwamba ndiye anayewatuma vijana nje ya nchi kupeleka madawa ya kulevya.