KHADIJA KOPA AZINGIRWA NA UMATI WA WATU KARIAKOO BAADA YA KUAMBATANA NA "SHOGA"
MASKINI! Malkia wa Mipasho Afrika Mashariki na Kati, Khadija Omary Kopa amevamiwa na vijana wahuni wakitaka kumfanyia fujo kwa madai ya kukatiza mitaani akiwa ameongozana na ‘mwaume tata’.
Tukio hilo lilijiri maeneo ya Kariakoo, Dar wiki iliyopita ambapo vijana hao walianza kwa kuzomea wakitaka kumshika mwanaume huyo waliyedai alikuwa amevaa nguo za jinsia ya kike.
Alichokifanya Khadija ni kuingia kwenye gari na kumwambia dereva aondoke haraka kukwepa kufanyiwa vurugu huku mwanaume huyo naye akiungana na malkia huyo kuondoka eneo hilo.
Wakizungumza na gazeti hili, vijana hao walidai kuwa Khadija alijiabisha kwa kuongozana na mwanaume huyo.
Khadija aliliambia gazeti hili kuwa alishangazwa na tukio hilo lililomkuta na kusema kuwa mwanaume aliyeongozana naye ni mwimbaji mwenzake ambaye pia ni shemeji yake.
Khadija aliliambia gazeti hili kuwa alishangazwa na tukio hilo lililomkuta na kusema kuwa mwanaume aliyeongozana naye ni mwimbaji mwenzake ambaye pia ni shemeji yake.
Alifunguka: “Hivi kuwa mwimba taarabu wa kiume ndiyo ushoga jamani? Au kuvaa kaptura ya kitenge ni tatizo? Mbona alikuwa amevaa mavazi mazuri tu ya kiume?”
Khadija alisema kuwa amewazoea mashabiki wake wa Kariakoo kwani huwa wakiwaona mastaa huwa na tabia hiyo na ndiyo maana walianza uzushi huku wakisema kuwa waimba taarabu wote ni wanawake, kitu ambacho si kweli.
“Sikuona sababu ya kuchukua hatua, nilikuwa najaribu kuwaelewesha lakini hawakunielewa, wakazidi kuzomea na kutuzingira ndiyo maana tuliamua kuondoka,” alisema Khadija.
GPL.
Posted by
Unknown

Related Articles
- MBUZI AZAA MTOTO MWENYE SURA YA BINADAMU HUKO KENYA
- ANGALIA KIDUME HUYU ALIVYOJICHUBUA NA KUWA KAMA KA BINTI
- HAWA NDIO WANAWAKE WA PETER NA PAUL OKOYE, WAMEPENDEZAJE?!!
- MASHABIKI WAMDISS MSANII HUYU KWA KUONGEZA UKUBWA WA MAKALIO NA MAT1TI
- PICHA YA LEO, NANI KATOKELEZEA ZAIDI
- JIMAMA LAFANYA BIASHARA YA UKAHABA MCHANA KWEUPEE, SIGARA MDOMONI, POMBE MKONONI NA KIVAZI CHA UTUPU.
- SHABIKI WA MAN U KENYA AJIUA BAADA YA KIPIGO CHA NEWCASTLE
- BAADA YA MBURUNDI KUSHINDA TUSKER PROJECT FAME SHANGWE ZA KWAO ZIMEKUWA HIVI
- MWANGALIE MODEL HUYU AKIWA NDANI YA BIK1NI NA KAPTURA WAPI KAPENDEZA ZAIDI