Polisi Mlevi Auwa1, na Kujeruhi 3 kwa Risasi Akiwemo Mjamzito.



Koplo Mohamed Abubakar wa MOPOL 17, Akure, Jimbo la Ondo katika Mji wa Festac anasakwa na Polisi baada ya Kuuwa Raia Mmoja na Kuwajeruhi Raia wengine watatu na Mama Mjamzito mmoja kwa kutumia silaha.

Walioshuhudia tukio hilo wamesema yalizuka mabishano kati ya baadhi ya Raia hao na Askari katika Mgahawa mmoja wa Chakula Mjini hapo, baada ya Askari huyo kupandwa na hasira alichukua silaha hiyo na kuwafyatulia Risasi Raia hao na kisha kutoroka eneo hilo.

Majeruhi wengine wanaendelea vizuri akiwemo mjamzito huyo na wataruhusiwa kwenda nyumbani hivi karibuni ingawa mmoja wao anhitaji afanyiwe Upasuaji.

Kamanda wa Polisi wa Jimbo Hilo Bw. Umar Manko amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na ameshangazwa na kitendo cha askari huyo wa Gari kutoka kitongoji cha Akure Kuwa Lagos Muda huo na Mpaka akafanya mauji na kujeruhi Raia Hao.

Juhudi za Kumsaka Koplo huyo zinaendelea.


Join Swahili One Community, "Like" and you will be one of us forever

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Copyright © 2013. swahili one Blog - All Rights Reserved
Customized by: Grace Tommy The One | Powered by: BS
Designed by: Creative Blogger