Mwalimu apigwa miaka 5 jela kwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanafunzi wake.
Jeremy Forest amehukumiwa kifungo cha miaka 5 na nusu jela baada ya kukubali mashtaka yaliyokuwa yakimkabili mwalimu huyo wa Hisabati, Mwalimu huyo wa miaka 30 amehukumiwa kwa makosa ya kumteka binti wa miaka 15 kisha kutoroka nae na kukimbilia Ufaransa ambapo waliponda raha za dunia kwa siku 8. Jana akiwa mahakamani hapo jamaa alithubutu kumwambia binti huyo " i love you" na binti akajibu " i love you too, im so sorry"
Kwa ishara za midomo huku binti akitoa machozi. Kwa upande wake msichana huyo ametetea uamuzi wake wa kwenda na mwalimu huyo kwamba hakulazimishwa na ya kwamba wanapendana.
Imeelezwa kuwa jamaa alianza uhusiano na mwanafunzi huyo akiwa na umri wa miaka 14, na aliwahi kumbusu darasani na ndipo mambo yakaanza rasmi. Pia katika ziara yao ya huko Ufaransa wamekuwa wakifanya mapenzi hadi mara 8 kwa siku moja ikiwa ni hotelini na katika gari.