Amvunja Mikono na Kumtoa macho mama yake Mzazi, Alimfananisha na Paka.
Tukio la Unyama wa aina yake umefanywa na Mwanamke aliyetambulika kwa jina la Ferna Quesner, 34 amemjeruhi mama yake mzazi baada ya kumkokota kupitia nywele, kumvunja mikono na pua na kisha kumtoa macho kwa kutumia kisu.
Macho ya mama huyo bi. Blonia Quesner, 59, yalikutwa karibu na bwawa la damu pembeni yake pamoja na kisu hicho. Polisi walipigiwa simu na majirani huko Lake Worth na walipofika walimkuta Fena amesimama akiwa katapakaa damu na mama yake akiwa chini hana fahamu huku damu zikimtoka.
Ferna amepelekwa katika kituo maalua cha kumchunguza kuhusu matatizo ya akili ambayo aliwahi kuwa nayo mnamo November 2001. Bado hali ya mama yake ni mbaya huko hospitali.