Angalia Picha 20 za Makamuzi ya Diamond Serena Hoteli katika Kulikaribisha Kombe la Dunia


Few hours ago,nchi yangu Tanzania imepata bahati  nyingine tena ya kutembelewa na ,kombe la dunia atakalo pewa mbabe wa kabumbu Duniani ,ni kombe linaloheshimika  sana duniani kote..Hafla ya kulipokea
imefanyika usiku  huu ndani ya viwanja vya hotel ya Serena jijini Dar ,na Diamond kama balozi wa Coca cola alikuwepo na alipangwa kama mmoja ya wasanii wa Kitanzania aliyetumbuiza
angalia picha zaid hapa........


Home sweet home,akijiandaa.........

My personal security officer,call him Mwarabu akiwa satandby kabisa akinisubili...

 Baada ya kuwasili hotelini@Serena hotel,kulikwa
 na ulinzi wa hali ya juu sanaa.........
                                      Akikwea ngazi kuelekea kwenye vyumba 

                                      

                                                              Backstage with my boys.............
                                                             Kazi ikaanza kihivii.............!!!!




                                                           Kwani nani amenunaa........!!!!!!!!!!!
                                                                   Mwali mwenyewe...!!!


                                                   Hapa sasa.ngololo ngololo..!!!!!!!!!
                                         Aha aaha aaha aipooh..aah aipooh............!!!!!!!!!
                                                        Amemaliza

Mshindi wa "EBSS" ni Emanuel Msuya, Mzigo wa Milioni 50 kwake, Angalia Picha Hapa




Hatimaye EBSS kwa mwaka 2013 imefika tamati jana kwa fainali zilizofanyika ndani ya Escape 1 mikocheni na msanii Emmanuel Msuya kuibuka Mshindi.
Washiriki walioingia Tatu Bora kutoka kushoto ni Elizabeth Mwakijambile, Emmanuel Msuya na Mellisa John.
Emmanuel Msuya akilia machozi ya furaha baada ya kuingia Tatu Bora.
Washiriki Elizabeth Mwakijambile, Emmanuel Msuya na Mellisa John wamefanikiwa kuingia Tatu Bora katika fainali za EBSS 2013 ndani ya Escape 1, Mikocheni jijini Dar muda huu. Wasanii walioaga…
Washiriki walioingia Tatu Bora kutoka kushoto ni Elizabeth Mwakijambile, Emmanuel Msuya na Mellisa John.
Emmanuel Msuya akilia machozi ya furaha baada ya kuingia Tatu Bora.



Washiriki Elizabeth Mwakijambile, Emmanuel Msuya na Mellisa John wamefanikiwa kuingia Tatu Bora katika fainali za EBSS 2013 ndani ya Escape 1.

Hivi ndivyo Mauti yalivyomfika Muigizaji wa Filamu za Fast and Furious, Paul Walker, Angalia Picha zaidi Hapa.



Muigizaji Paul Walker , anayejulikana  sana duniani kwenye uigizaji kupitia filamu za Fast and Furious , amefariki katika ajali ya gari.

Ajali hiyo imetokea katika eneo la Santa Clarita, kaskazini ya Los Angeles wakati alipokuwa katika tukio la kijamii.

Walker alikuwa ni abiria katika gari aina ya  Porsche kwamba waliopotea kudhibiti na kugonga ama taa ya posta au mti kabla ya kupasuka ndani ya moto .

Kifo muigizaji baadaye kilithibitisha  kwenye ukurasa wake wa Facebook  .

Taarifa kwenye  ukurasa huo  zilisema:

 " kwa moyo  mnzito kwamba tunapenda kuthibitisha kwamba Paulo Walker amefariki leo katika kutisha ajali ya gari wakati akienda kuhudhuria tukio upendo kwa shirika lake kuwasaidia watu duniani kote.

"Yeye alikuwa ni abiria katika gari ya rafiki yake, ambayo wote walipoteza maisha yao .

"Asante kwa ajili ya kuweka familia yake na marafiki katika maombi yako katika wakati huu mgumu sana .



 View image on Twitter
2013-11-30_2220
Mtandao wa TMZ umeripoti kwamba Star uyo alikuwa katika harakati za kuchangia mfuko kwa watu wa taifa la Philippines waliokubwa na mafuriko yaliyosababisha kuwapoteza ndugu zao pamoja na makazi, pia  kilieleza kwamba katika gari Walker alikuwa anaendeshwa na dereva wake ambapo yeye alikuwa amekaa katika siti ya abiria, katika ajali iyo hakuna aliyeweza kutoka mzima.                                                                               
RIP PAUL WALKER

Mshiriki wa Tusker Project Fame Kutoka Tanzania Azidi Kung'ara


 Mshiriki toka Tanzania anayetuwakilisha kwenye mashindano ya Tusker project fame amefanikiwa kusonga mbele kwa mara nyingine baada ya kuwa kikaangoni  yeye pamoja na washiriki wenzake wote ndani ya Tusker project fame.Waliotoka wiki hiii ni Phiona toka Rwanda na Kojjo kutoka Uganda.Hongera Hisia Tanzania Gooooooooooooooooo Goooooooo

Ripoti kuhusu Mishahara ya Vigogo, Ipo Juu kulingana na Ufanisi wao.



Rais Jakaya Kikwete alinukuliwa katika kikao cha OGP London akisema mishahara ya viongozi wa umma haiwezi kuwa siri kwani ni sehemu ya bajeti, ingawa leo hii wengi katika serikali yake wanatetea usiri uliokithiri katika suala zima la vipato vya ‘wakubwa.’


Ripoti mpya ya utafiti imebainisha kuwa mishahara mikubwa wanayolipwa viongozi wa juu serikalini na wanasiasa hailingani na utendaji wao wa kazi.
Ripoti hiyo iliyozinduliwa jana jijini Dar es Salaam, imeeleza kuwa viongozi hao wanalipwa mishahara inayotofautiana kwa kiwango kikubwa na pato la mwananchi wa kawaida.
Huku ikitaja mapato ya mishahara ya marais wa baadhi ya nchi za Afrika Mashariki ikiwamo Tanzania, imesema kuwa hali hiyo ni kuibebesha jamii mzigo wa kugharimia malipo ya viongozi.
Akizindua ripoti hiyo iliyochunguza gharama za kuwalipa viongozi wa Serikali na wanasiasa, Mtafiti kutoka Taasisi ya Utafiti kuhusu Kuondoa Umaskini (Repoa), Dk Theodore Valentine, alisema kuwa viongozi wa Afrika Mashariki ndio wanaoongoza kwa kulipwa mishahara mikubwa zaidi chini ya Jangwa la Sahara.
“Kama viongozi wakuu watakuwa wanalipwa mishahara mikubwa, nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara zitaweza kugharimia demokrasia?” alihoji Valentine.
Utafiti huo uliofanyika kati ya mwaka 2009 na 2012, umebainisha kuwa Rais wa Tanzania analipwa mshahara dola 172,014 kwa mwaka (Sh275 milioni) sawa na Sh22.9 milioni kwa mwezi, huku Rais wa Kenya, akiongoza kwa kulipwa dola 515,021 kwa mwaka (Sh824 milioni) kwa mwaka sawa na Sh68.6 milioni kwa mwezi.
Rais wa Rwanda analipwa dola 199,000 kwa mwaka (Sh124 milioni) sawa na Sh10 milioni kwa mwezi, wakati rais wa Nigeria akipokea dola 161,902 (Sh259 milioni) ambazo ni sawa na Sh21 milioni kwa mwezi.
Pia umeeleza kuwa Rais wa Kenya analipwa mara 320 zaidi ya pato la mwananchi wa kawaida wa nchi hiyo, wakati rais wa Afrika Kusini anapata mara 46 na Rwanda mara 150 zaidi ya mwananchi wa kawaida.
Ripoti hiyo imeendelea kubainisha kuwa rais wa Tanzania analipwa mara 8.2 ya mshahara wa hakimu, huku rais wa Kenya akipokea mara 13.1 na kumpita rais wa Rwanda anayechukua mara 12 zaidi ya mshahara wa hakimu.
Kwa upande wa wabunge, utafiti huo umeeleza kuwa wabunge wa Tanzania wanalipwa mara 3.0 ya mshahara anaolipwa hakimu, Kenya (5.5) na Rwanda (3.0). Viwango hivyo vimetajwa kuwa vikubwa kuliko vya wabunge wa Nigeria na Afrika Kusini.
Naibu Spika anena
Naye Naibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Job Ndugai alisema kuwa umefika wakati ambapo mishahara ya viongozi wa umma inabidi iwekwe wazi kwa wananchi.
“Ningependa mishahara ifahamike kama ilivyo kwa nchi nyingine, hii itaondoa uongo kwa wabunge,” alisema.
Alisema mishahara wanayolipwa wabunge siyo mikubwa na kwamba inapaswa kuongezwa zaidi kwa kuwa hivi sasa imetofautiana kidogo na ya wakuu wa wilaya.
“Mshahara wangu mimi kama Naibu Spika ni mdogo…, hata wa Waziri Mkuu siyo mkubwa. Siku zote mtu anapoongezewa mshahara inamwongezea motisha ya kufanya kazi,” alisema Ndugai.
Serikali yajibu
Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk Makongoro Mahanga, alisema viongozi wanalipwa mshahara kutokana na nyadhifa walizonazo, hivyo haoni sababu ya jambo hilo kujadiliwa.
Alisema mshahara ni siri ya mfanyakazi husika, na kwamba iwapo itawekwa wazi baadhi ya watu wataacha kujadili mambo ya maendeleo na badala yake wataanza kuzungumzia malipo hayo.
“Tujadili kuhusu namna ambavyo gesi itatuletea maendeleo kwenye uchumi wa nchi yetu na siyo mishahara,” alisema.
Alipopigiwa simu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Hawa Ghasia, alihoji kuwa anazungumza na nani, mwandishi alipojitambulisha alitaka apewe muda hadi baadaye kwa madai kuwa hakuwa sehemu nzuri.
Rais Kikwete na OGP
Akinukuliwa na gazeti la Serikali, Rais Jakaya Kikwete, ambaye Oktoba 31 hadi Novemba Mosi 2013, alihudhuria Mpango wa Pamoja wa Uendeshaji wa Serikali kwa Uwazi (OGP) uliofanyika London, Uingereza, ambapo alizungumzia uwazi kwenye Serikali yake likiwemo suala la mishahara.
Mkutano huo ulihudhuriwa na washiriki 1,000 kutoka nchi 60 wanachama na Rais Kikwete alipata nafasi ya kuuelezea mkutano huo, namna Tanzania ilivyoanza utekelezaji wa masharti ya mpango huo.
Rais Kikwete alisema kuwa mshahara wa mtumishi wa umma hauwezi kuwa siri na ndiyo maana unawekwa katika bajeti ya serikali.
“Mishahara haiwezi kuwa siri. Si ipo kwenye bajeti za Serikali?” Alijibu Rais Kikwete alipoulizwa kama suala la mishahara litaendelea kuwa siri katika utekelezaji wa mpango huo.
Rais Kikwete alisema: “Changamoto iliyopo ni kwamba mpango huu unabadili mazoea yetu ya kufanya kazi. Sisi katika kila Serikali kila kitu kilikuwa siri. Sasa OGP inataka mambo haya yawe wazi, ifike hatua mtu aone kutoa habari ni wajibu.”
TUCTA yatoa kauli
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA), Nicolas Mgaya alisema wabunge wanalipwa mishahara mikubwa lakini baadhi yao hawaonekani kwenye vikao.
Alitaka mishahara yao iwekwe wazi kwa wananchi kwa kile alichokieleza kuwa kwa sababu wanalipwa kwa kutumia kodi za wananchi.
Anavyosema Profesa Wangwe
Akizungumzia matokeo ya utafiti huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Repoa, Profesa Samuel Wangwe alisema kuna haja ya kuangalia gharama za kuwalipia viongozi.
“Tuangalie gharama ya demokrasia, lakini jambo la msingi ni kuwa kama wabunge wanalipwa kiasi kinachotajwa basi wafanye kazi yao wanayostahili na wasisahau kwamba wanawawakilisha wananchi ambao ni maskini,” alisema.
Profesa Lipumba
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi - CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, ambaye ni mchumi kitaaluma alisema kuwa hakuna ushahidi unaoonyesha kuwa viongozi wakilipwa mishahara mikubwa wanafanya kazi zaidi.
“Hakuna ushahidi wowote kwamba kwa kuwalipa wabunge mishahara mikubwa basi wanafanya kazi vizuri zaidi,” alisema.
Akitolea mfano wabunge wa Kenya alisema: “Katika kipindi cha miaka mitano mbunge wa Kenya analipwa dola za Marekani dola 1milioni (sawa wa Sh1.6 bilioni) kiasi ambacho ni sawa na Sh26 milioni kwa mwezi.”
Aliongeza kuwa mishahara ya wabunge wa Tanzania ni zaidi ya mara 40 ya pato la kawaida la mwananchi.
Alipendekeza kuanzishwa kwa taasisi ambayo itapewa jukumu la kusimamia mapato ya viongozi wa umma, na kwamba ni vyema katiba izungumze kuwa mishahara na marupurupu ya wabunge itapangwa na taasisi ambayo ipo huru itakayozingatia mapato ya nchi yalivyo.
Mwananchi


SAKATA LA PICHA ZA "UTATA" ZA AISHA MADINDA, MILIONI 500 NJE NJE.


Kampuni ya Global Publishers Ltd, inayochapisha magazeti ya Uwazi, Championi, Ijumaa Wikienda, Risasi, Amani na gazeti hili, iko tayari kumlipa kiasi cha shilingi Milioni mia tano, mnenguaji wa Bendi ya Twanga Pepeta, Aisha Mohamed Mbegu ‘Aisha Madinda’ ikiwa atatoa uthibitisho kwamba, picha za u2pu alizopigwa nchini Afrika Kusini ni za kutengenezwa, soma data chini.

Ofa hii imekuja siku mbili baada ya gazeti moja la michezo na burudani linalotoka mara mbili kwa wiki, toleo la Jumanne Mei 18, 2010 kuchapisha makala kuhusu Aisha akikanusha kuwa, picha zile si zake na kwamba zilitengezwa na mbaya wake kwa lengo la kumchafua jina.
...kulia kwake ni unga..bila shaka ulimpotezea kumbukumbu

Hata hivyo, katika makala hayo, Aisha alishindwa kuthibitisha picha hizo ni za kutengeza, zilitengnezwa wapi na lini na vigezo gani vinavyoonesha picha hizo ni za kutengeneza.

Ushahidi wa Global kuwa, picha hizo ambazo za mnato na video ni za Aisha mwenyewe upo wazi na hakuna shaka yoyote.

Moja ya ushahidi huo, katika picha za video, kuna sehemu Aisha anaongea kwa tambo akiwaponda watu wanaomfuatafuata na kumsema vibaya.0
...sasa hapa inakuwaje picha hizi zikitoka gazetini...!!!!
Tunamnukuu: “Wanasema eti nimeishiwa, nimekosa nauli ya kurudi Tanzania, waende basi kwa huyo Asha Baraka wakaseme, maana wamezidi kwa maneno.” 

Hata hivyo, sehemu kubwa ya picha za mnato na video hizo zinaonesha wazi kwamba, Aisha alikuwa tayari kupigwa picha hizo, kwani kuna wakati alikuwa akitazama kamera na nyingine akiwa ameweka pozi.
......aaa jamani...niacheni ki mpango wangu!!!!

Aidha, ushaidi mwingine kuwa picha hizo ni Aisha, mara baada ya kutua Bongo akitokea Afrika Kusini, alimwangukia bosi wake, Asha Baraka akimwomba radhi kwa yote aliyoyafanya Afrika Kusini ambapo gazeti hili liliripoti likiwa na kichwa cha habari; NATESEKA.

Katika habari hiyo, Asha Baraka ‘Iron Lady’ alinukuliwa akisema kuwa, anaamini Aisha aliteleza na hivyo ameamua kumsamehe na kumrudisha kundini kuendelea kupiga mzigo kama kawa.
....ntajua ntakachowaeleza watanzania....

Tunamnukuu Asha Baraka: “Mimi kwa Aisha ni kama mama au dada yake, na ninavyojua, mtoto anapojisaidia kiganjani mzazi huwezi kuukata mkono bali utausafisha kisha kuyaacha mambo yaendelee. Vivyo hivyo kwa Aisha, kafanya kosa lakini hakuna kosa lisilostahili msamaha, kwahiyo asamehewe.

“Atakachokifanya Aisha ni kuomba radhi kwa mashabiki wake na katika kila sehemu ambayo tutafanya shoo atafanya hivyo kabla ya kuanza kutumbuiza.” 
.......ni mzimu wangu tu huu...siyo mimi..!

Pia, katika kuonesha ubinadamu, mwisho wa habari hiyo Mhariri aliwaomba Watanzania wasahau yaliyopita kuhusu Aisha na aombewe kwa Mungu ili amwepushe na mitihani mingine nkatika maisha yake.

Katika hali ya kushangaza sana, baada ya kimya cha muda mrefu, Aisha ameibuka katika gazeti hilo akidai kwamba picha zile zilikuwa za kutengeneza hali iliyozua maswali miongoni mwa wasomaji wetu.

Habari hiyo, ambayo ilionekana Aisha alikuwa amelenga kuwafanya Watanzania waamini Ijumaa linaandika habari za ‘mezani’ alisema, yupo mwanaume mmoja aneyemsumbua kimap3nz! kwa muda mrefu, ambaye ndiye aliyemfanyia unyambisi huo.
......mimi siyo Aisha niangalieni vizuri...!!!!!

“Huyo anayenichafua alikuwa ananitaka kimapenzi nikamkatalia na siwezi kumkubalia, hata kwa mtutu simpi mwili wangu ng’o, kuamua kunitangazia sifa chafu si suluhisho la mimi kumkubali, zaidi ya kumuona kichekesho kwani katika jamii ya watu wastaarabu hafai, namfananisha na ‘nungayembe’ la kiume,” alisema Aisha katika sehemu ya habari hiyo.

Aidha, aliongeza: “Picha za ng0n0 zilizoenea kila kona ya nchi, zinazonihusu mimi si za kweli, amefanya hivyo kwasababu ‘nilimpiga za uso kavukavu bila chenga’, siwezi kupoteza muda wangu kubishana naye, nitakuwa nampandisha chati, lakini ajue hata kwa mtutu hapati kitu kwangu.” 

Katika juhudi za kulishusha ‘grade’ gazeti hili, sehemu ya habari hiyo ilisomeka, ‘Anadai amekuwa akikabiliwa na tuhuma za kupiga picha za ng0n0 na u2pu zilizosambazwa sehemu mbalimbali hasa katika magazeti ya udaku, ambapo kiuhalisia si zake.
....baada ya mitungi, mikasi....Aisha akiwa na Khumalo
Katika hatua nyingine, mapema wiki hii, kijana Khumalo aliyefanya naye uchafu huo nchini Afrika Kusini, amelitumia waraka pepe (e-mail) gazeti hili akiomba msahama kwa Aisha.


Alisema anakiri kumtenda vibaya (kupiga na kulikisha picha hizo) mnenguaji huyo, lakini anamuomba amsamehe na waanze ukurasa mpya

credit:mjizzo


Join Swahili One Community, "Like" and you will be one of us forever

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Copyright © 2013. swahili one Blog - All Rights Reserved
Customized by: Grace Tommy The One | Powered by: BS
Designed by: Creative Blogger