HIVI NDIVYO JINSI WEMA "ANAVYOMMISS" BABA YAKE
MADAM, Wema Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ amesema anakumbuka vitu vitatu muhimu alivyokuwa akifanyiwa na marehemu baba yake, Abraham Sepetu.
Akizungumza na paparazi wetu, Wema alitaja matukio hayo ambayo ni kuona simu ya baba yake ikimpigia katika simu yake, jinsi alivyokuwa akimbembeleza na kubwa zaidi ni uwepo wake pia kwa jumla.
“Maisha yangu yote nitakumbuka vitu vitatu ninavyovikosa baada ya kifo cha baba yangu, kwanza uwepo wake, kuona simu yake pindi anipigiapo, na alivyokuwa akinibembeleza. Nitamkumbuka sana baba yangu,” alisema Wema.