NILIPELEKWA MUHIMBILI ILI NIINGIZWE MOCHWARI
INAWEZEKANA wapo wagonjwa wanaopelekwa chumba cha kuhifadhia maiti (mochwari) wakiwa hai. Huenda wengine hufia humo baada ya kuzidiwa na baridi la chumba hicho sambamba na kukosa hewa. Piga picha ni wewe!
Lakini kwa kijana Anina Shaban (28) mkazi wa Kijiji cha Mbugu Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro, yeye alibahatika, kwani aliishia kwenye lango la kuingia mochwari akidhaniwa ameshakufa.
Akizungumza na mwandishi wetu hivi karibuni akiwa ndani ya wadi ya Sewa Haji kitengo cha MOI katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar alikolazwa kwa miezi 9 sasa, Anina anasema:
“Siwezi kuisahau siku ile, ninachoweza kusema kwa urahisi sana ni Mungu tu ndiye aliyependa nisife kwa wakati asiokubaliana nao, vinginevyo leo ningekuwa kaburini.
“Ilikuwa mwezi wa tatu, tarehe ishirini na nne nakumbuka, siku hiyo nilitua hapa Dar kwa mara ya kwanza nikitokea kijijini kwetu.
“Lengo la kuja Dar lilikuwa kutafuta maisha mazuri, maana vijana wenzangu waliotangulia kuja kila waliporudi kusalimia waliniambia maisha bora yapo kwenye Jiji la Dar es Salaam.
“Lengo la kuja Dar lilikuwa kutafuta maisha mazuri, maana vijana wenzangu waliotangulia kuja kila waliporudi kusalimia waliniambia maisha bora yapo kwenye Jiji la Dar es Salaam.
“Niliamini kwani hata mavazi yao yalionesha kwamba kweli wana maisha mazuri. Sasa ni nani asiyetaka maisha mazuri? Ndipo nikaamua kuja Dar siku hiyo.
“Lakini ndoto zangu ziligonga mwamba mara tu niliposhuka Kimara. Nilivuka barabara kwenda upande wa pili nikiwa na begi langu lenye nguo mbili tatu, ghafla daladala lilitokea na kunigonga, nikaanguka na kupoteza fahamu! Ilikuwa ajali kubwa sana.
“Nilipopata fahamu nilijikuta nikiwa hapa Muhimbili, lakini nikiwa katika hali isiyokuwa ya kwangu, mikono, miguu ilifungwafungwa. Nilianza kulia huku nikiwa sijui hapa ni wapi.
“Daktari mmoja alipita na kuniona nikilia, akaja na kuniuliza kilichoniliza, nikamjibu hali nilionayo, ndipo akanisimulia kwamba nilipata ajali mbaya sana Kimara wakati nikivuka barabara.
“Kilichonishangaza zaidi ni pale nilipomuuliza ajali hiyo ilitokea lini, akaniambia mwezi mmoja uliopita. Ina maana mimi nilikuwa katika hali ya kutojitambua kwa muda wote huo.
“Cha ajabu, aliniambia nilifikishwa hapa si kama majeruhi bali kama maiti ya mtu aliyekufa kwa kugongwa na gari.
“Daktari huyo alisema walionileta kila mmoja alijua nimeshaaga dunia kufuatia ajali ile. Hivyo nilikuwa napelekwa moja kwa moja mochwari.
“Daktari huyo alisema walionileta kila mmoja alijua nimeshaaga dunia kufuatia ajali ile. Hivyo nilikuwa napelekwa moja kwa moja mochwari.
“Daktari aliendelea kunieleza kuwa hakuna aliyejua kwamba bado nilikuwa hai kwani nilikuwa siangaliki kutokana na majeraha makubwa niliyoyapata.
“Hata hivyo, kabla sijaingizwa mochwari daktari mmoja alitaka kujiridhisha kwanza kama kweli nilishafariki dunia, ndipo akagundua kuwa bado nilikuwa hai kwani nilikuwa napumua kwa mbali sana.
“Nilikuwa nimeumia vibaya mno. Nilivunjika mikono yote, tena mara mbilimbili, nilivunjika miguu yote na mbavu tatu.
“Nilifikishwa hospitalini nikiwa nimekunjwa kama mtu anavyobeba nyama kwenye mfuko wa rambo. Mwacheni Mungu aitwe Mungu jamani, siamini kama kweli leo hii naweza kukaa mwenyewe.
“Nilifikishwa hospitalini nikiwa nimekunjwa kama mtu anavyobeba nyama kwenye mfuko wa rambo. Mwacheni Mungu aitwe Mungu jamani, siamini kama kweli leo hii naweza kukaa mwenyewe.
“Nilijiuliza nilipata wapi mkosi huo? Mbona niliwaaga vizuri tu wazazi wangu kwamba nakuja Dar kutafuta ajira na walinikubalia kwa vile katika watoto watatu katika familia yetu, mimi ndiyo mtoto wa kwanza na wote tulikuwa nyumbani tukiendelea na kilimo cha jembe la mkono.
“Nilijua hapa Dar ningepata kibarua hata cha kuwakatia ng’ombe majani au kuwasombea wajenzi matofali lakini kwa bahati mbaya sikuyafikisha malengo niliyoyakusudia.
“Kinachoniuma na kunitoa machozi ni kuwaona wagonjwa wenzangu wanatembelewa na ndugu zao, wanawafariji na kuwaletea vyakula lakini kwa upande wangu hakuna hata mmoja.
“Kule kijijini wazazi hawana simu, mimi hapa pia sina simu, ni vigumu kuwajulisha, nahisi wanaamini tayari nimeshapata kibarua lakini siwakumbuki.
“Wangejua wangenifuata kunichukua na kunirudisha kijijini kwetu,” Anina alisema na kuanza kulia.
“Wagonjwa tuliolazwa nao wengi wameshapona na kuruhusiwa kurejea makwao. Lakini nasikitika kwamba nilitoka nyumbani mzima nitarudi na ulemavu,” akalia tena.
“Wagonjwa tuliolazwa nao wengi wameshapona na kuruhusiwa kurejea makwao. Lakini nasikitika kwamba nilitoka nyumbani mzima nitarudi na ulemavu,” akalia tena.
“Nitakwenda kuwapa wazazi wangu kazi ngumu ya kunitunza kama mtoto mdogo, hakuna jinsi inabidi niyakubali matokeo, najua huu ndiyo mwisho wangu wa utafutaji, nimebakia mtu wa kitandani, sikuyapenda maisha haya bali ndivyo Mungu alivyonipangia natembea lakini si kama zamani,” alisema kijana huyo.
Aliwaomba Watanzania ambao wangependa kumsaidia watumie namba hii 0713 413098.
Naye Afisa Mkuu Msaidizi Mambo ya Jamii Kitengo cha Mifupa MOI, Matua Frank alisema Anina anaendelea vizuri na wakati wowote wanaweza kumsafirisha kwenda kwenda kijijini kwao.
Naye Afisa Mkuu Msaidizi Mambo ya Jamii Kitengo cha Mifupa MOI, Matua Frank alisema Anina anaendelea vizuri na wakati wowote wanaweza kumsafirisha kwenda kwenda kijijini kwao.
“Kwa sasa tunajiandaa kumsafirisha, tumempatia matibabu kwa kipindi chote hicho kwa gharama ya hapa hospitali hadi sasa amepata nafuu kwa kiasi fulani,” alisema Frank.
GPL