Mugabe Mlalavi Mikutanoni
Waziri katika serikali ya muungano ya Zimbabwe Bw Ncube amelalamikia vitendo vya Rais Huyo kuwa Mchapaji mzuri wa Usingizi katika Vikao hasa vya SADC, na kwamba muda umefika kwa Rais huyo kuachia ngazi. Amesema chukulia mfano mtu aliyezaliwa mwaka 1980, mpaka leo ana miaka 32, na bado kichwani kwake anamjua Rais huyo huyo tu, mbona wakina Kwame Nkurumah, Samora Machelle na Mandela walikubali kuachia ngazi, muda umefika Wazimbabwe kujua ni nani watamweka katika nafasi hiyo ambaye atawaongoza na atabadilisha Taswira ya Nchi yao.