Kutana na Afande "Mrembo"

Kwa kumtazama haraka haraka unaweza dhani ni kama muigaziji hivi katika tamthilia fulani, kumbe ni Afande wa Polisi nchini Nigeria, Ngozi Conchita, mwanadada huyo ameweka historia kwa kuwa Afisa Uhusiano wa Kwanza wa kike wa Jeshi hilo Kanda Ya Lagos, huku akiwa ni wa 16, kushika nafasi tangu kuundwa kwa jeshi hilo. Mbali na nafasi hiyo ameshawahi kushiriki katika kikosi maalum cha kulinda amani Nchini Liberia mwaka 2006, pia amewahi kuwa katika idara nyeti kama za Interpol na idara ya Magendo. Mwanadada huyo alijiunga na jeshi la Polisi mwaka 1996 baada ya kuhitimu Shahada yakee ya kwanza ya Lugha kutoka Chuo kikuu cha Lagos.

Join Swahili One Community, "Like" and you will be one of us forever

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Copyright © 2013. swahili one Blog - All Rights Reserved
Customized by: Grace Tommy The One | Powered by: BS
Designed by: Creative Blogger