Kumekucha "BONGO MOVIE", Nisha naye Akimbia na Samani za Ndani za Rafiki yake.

-->



Na Gladness Mallya
MSANII wa filamu za Kibongo, Salma Jabu ‘Nisha’ ametupiwa tuhuma nzito za utapeli wa samani za ndani baada ya kupewa hifadhi na shoga’ke aitwaye Amina Mrisho anayeishi Ilala jijini Dar, Ijumaa limetonywa.
Salma Jabu ‘Nisha’.
Kwa mujibu wa Amina, tukio hilo limetokea mwaka 2011 baada ya msanii huyo kukosa fedha za kulipia kodi na kuomba hifadhi kwake.
“Alitakiwa kuondoka katika nyumba aliyopanga akaomba hifadhi kwangu nikamsitiri kwa kuwa alikuwa ni rafiki yangu, akahamia na vitu vyake vyote vya ndani,” Amina alianza kushusha madai hayo na kuendelea:
“Baada ya muda alitangaza kuziuza samani zake kwa shilingi 750, 000 ili apate fedha za kuendeshea maisha, nikaahidi kuzinunua na nikamtangulizia shilingi 500,000 kama malipo ya sofa, meza ya runinga, dressing table na meza ya jikoni.”
Hata hivyo, msichana huyo alisema kwamba kabla mwezi haujaisha, Nisha alibadilika na kutaka fedha zilizobaki kwa nguvu huku akimpa vitisho kwa kumwambia kuwa atamkomesha kwa kuwa risiti zote za samani hizo alikuwa nazo.
Amina Mrisho.
Inazidi kudaiwa kwamba Nisha alienda kutoa taarifa polisi na kudai kwamba Amina alimwibia samani zake.
“Pamoja na kujieleza polisi muafaka ulifikiwa kwamba Nisha achukue samani zake na miye sikuambulia chochote,” alisema Amina.
Baada ya malalamiko hayo, paparazi wetu alimtafuta Nisha ili kupata ukweli, naye alikuwa na haya ya kusema:
“Kwanza huyo Amina simfahamu na katika maisha yangu sijawahi kukaa kwa mtu kwa sababu ya kuishiwa hela ya kulipia kodi. Mama yangu ana nyumba kubwa tu, ningewezaje kuiacha na kwenda kukaa kwa mtu baki?”
“Ukishafanikiwa lazima kuna watu wataibuka na kusema maneno mabaya ili wakushushe kama huyu miye wala simfahamu ni muongo tu.”


SOURCE: GPL

Join Swahili One Community, "Like" and you will be one of us forever

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Copyright © 2013. swahili one Blog - All Rights Reserved
Customized by: Grace Tommy The One | Powered by: BS
Designed by: Creative Blogger