Mwanamke ajifungua mtoto akiwa na "TASBIH" Shingoni.
Maajabu mengine yametokea tena, baada ya mwanamke kujifungua mtoto mwenye kufanana na nyani, juzi tena amejifungua mwanamke mwingine mtoto akiwa na Tasbih (Kifaa cha kuvutia uradi kwa waislam) ikiwa shingoni.
Imeelezwa na nesi aliyemzalisha mwanamke huyo nyumbani kwao ya kwamba wakati wakiendelea na taratibu za kumpokea kiumbe huyo duniani, waliona kitu mfano wa kamba kimemzunguka shingoni kwa mtoto huyo huku kikiwa cheusi, hata hiyo baada ya kumtoa mtoto huyo kitu hicho kilibadilika na kuwa cheupe kama inavyoonekana katika picha
Miongoni mwa wazee wa Ki iman waliokuwepo eneo hilo wamesimulia kitendo hicho kama miujiza katika kuonesha uwezo wa Mungu (Allah)
Mama wa mtoto huyo ni Adijat aliyeolewa na Mallam Issa.