Unamkumbuka Rehema?!!, Sasa anakula bata na Mtoto wa Balozi Huko China!!
Na Hamida Hassan
MLIMBWENDE aliyewahi kung’ara katika Shindano la Miss Kiswahili 2009, Rehema Fabian anadaiwa kuangukia kimapenzi kwa mtoto wa Balozi wa Nigeria nchini China aliyemtaja kwa jina moja la Allen anayetaka kufunga naye ndoa.
“Nimechoshwa na masharobaro hivyo nimeamua kutulia na mwanaume huyo kwa sababu nimempenda na yeye anaonekana kunipenda,” aliandika Rehema.
Rehema ambaye kwa muda mrefu amekuwa nchini humo, alisema kwamba amekuwa akipata wanaume wanaomtumia na kumuacha lakini safari hii amepata mtu sahihi.
“Tumepanga kuja Tanzania kwa ajili ya kukamilisha mipango ya ndoa, hivyo nitarajieni huko muda si mrefu,” aliandika Rehema na kuongeza kwamba atafanya bonge la sherehe.
Source: GPL