Akimbiwa na Mumewe Baada ya Kujifungua Mapacha 3,


Pichani ni Mke wa Mkulimu kutoka Jimbo la Ogun, Bi Bosede Akapo, 30, Ambaye analalamikia kukimbiwa na mumuwe baada ya kujifungua watoto watatu mapacha siku ya tarehe 24/07/2013.

Imeelezwa kuwa Bw. Biodun mume wa mwanamke huyo alikimbia siku ambayo Bosede alianza kuumwa Uchungu wa Uzazi. Kabla ya ujio wa malaika hao watatu, tayari familia hiyo tayari ilikuwa ana watoto wawili hivyo kuifanya idadi ya watoto kuwa watano ambao wamempelekea Mkulima huyo kuingia mitini.

Mwanamke alipata msaada wa kuzalishwa na wazee wa kijijini kwake ambao walimsaidi kumpandisha Pikipiki na kumpeleka katika kituo cha afya na huko ndipo mambo yalipojulikana. Amesema hakuwahi kufanya Kipimo cha " Ultra Sound" kufahamu Watoto na Jinsia kwani hakuwa na uwezo huo.

Anamsihi mwanaume huyo kurudi nyumbani wailee familia hiyo kubwa ambayo peke yake haitaiweza.

Join Swahili One Community, "Like" and you will be one of us forever

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Copyright © 2013. swahili one Blog - All Rights Reserved
Customized by: Grace Tommy The One | Powered by: BS
Designed by: Creative Blogger