Ambaka Rafiki Yake Kisha kumpiga Picha za Uchi na Kuziweka katika Mitandao ya Kijamii.
Awali ya yote Tunampa pole Thelma Lawrance, Msichana wa miaka 23, mwanafunzi kutoka Chuo cha Masuala ya Kiteknolojia kwa mkasa uliompata baada ya Kubakwa na Rafiki wake wa kawaida alipokwenda kuchukua " Memory Card" yake.
Thelma, Alifanyiwa unyama huo na Henry Aiyenero, 27, ambaye siku zote alikuwa akimchukulia kama rafiki yake wa kawaida ingawa kwa mara kadhaa alikuwa akimtongoza na kumshawishi kuhusu kufanya mapenzi lakini akawa anakataliwa.
Siku ya Tukio Thelma alikwenda kuchukua Memory card hiyo kwa Henry, alipofika Henry aliwahi kuufunga mlango, kisha akamtolea kisu na kumwambia aidha kubali Kupigwa Picha za Uchi kupitia simu ya mwanaume huyo au ampe "Penzi"
Thelma alikubali kuvua nguo na kumwambia atampa Penzi lakini asimpige Picha, Henry akapewa alichokihitaji huku akiwa ameshikilia kisu chake mkononi na baadae akampiga picha na Video msichana huyo kisha akizirusha mtandaoni na ku share na rafiki zake.
Polisi Wameshamkamata mwanaume huyo, ingawa amekana mashtaka hayo yupo mahabusu kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana na kesi yake itasikilizwa tena tarehe 4 mwezi wa 9, 2013.