Mke Mtarajiwa Anaswa Akijiuza, Atupwa Gerezani hadi Agosti 20
ZA mwizi arobaini! Kauli hiyo ya wahenga ilitimia Jumatatu iliyopita kufuatia msichana Pili Baraka (21) aliyevishwa pete ya uchumba na mpenzi wake hivi karibuni (jina tunalihifadhi) kujikuta akitupwa Gereza la Segerea jijini Dar baada ya kunaswa kwa tuhuma za ukahaba, Amani linakupasha.
Mrembo huyo alifikishwa kwenye Mahakama ya Sokoine Drive (Jiji) na kusomewa shitaka na mwendesha mashitaka wa mahakama hiyo, Richard Magodi mbele ya Hakimu Timothy Lyon.
Akisoma shitaka hilo, Magodi alisema: Agosti 5, mwaka huu, saa nane usiku, Pili alinaswa kwenye maeneo ya Manzese jijini Dar akifanya biashara ya ukahaba.
Aliposomewa shitaka lake hilo, Pili aliinamisha kichwa na kujibu kwa kifupi: Si kweli.
Licha ya kukana shitaka hilo, Hakimu Lyon alimtaka mchumba huyo wa mtu kutafuta wadhamini wawili lakini aligonga mwamba na kupelekwa Gereza la Segerea mpaka Agosti 20, mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena.
Licha ya kukana shitaka hilo, Hakimu Lyon alimtaka mchumba huyo wa mtu kutafuta wadhamini wawili lakini aligonga mwamba na kupelekwa Gereza la Segerea mpaka Agosti 20, mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena.
Akijitetea kabla ya kupandishwa kwenye karandinga kwenda Segerea, Pili aliiomba mahakama hiyo imuonee huruma asiende kuilia Sikukuu ya Idd, Segerea kwa kuwa mchumba’ake yuko safarini kikazi na hakuwa na mtu mwingine wa kumwekea dhamana, ombi ambalo lilikataliwa.