Video ya Jambazi Lilloinusurika Kuuliwa na Raia wenye Hasira Huko Mbezi Dar Es Salaam



KIJANA mmoja ambaye hajafahamika jina lake anayedaiwa kuwa ni jambazi amenusurika kuuawa na wananchi wenye hasira kali eneo la Mbezi kwa Msuguli jijini Dar es Salaam. 


Kijana huyo pamoja na mwenzake wakitumia pikipiki walikuwa na silaha za moto tayari kwa kwenda kufanya uhalifu lakini kabla mpango wao haujakamilika polisi waliingilia kati na kuanza kupambana nao. 



Haikuwa kazi rahisi kuweza kumkamata jambazi huyo kutokana na majibizano ya risasi kati yake na polisi. 


Baada ya jambazi lililokuwa linaendesha pikipiki kuona mwenzake anaelekea kukamatwa lilitokomea wakati mwenzake akiangukia mikononi mwa wananchi wenye hasira kali waliomshushia kipondo cha nguvu.

TAZAMA  VIDEO  HAPO  CHINI....


Source: Mpekuz

Join Swahili One Community, "Like" and you will be one of us forever

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Copyright © 2013. swahili one Blog - All Rights Reserved
Customized by: Grace Tommy The One | Powered by: BS
Designed by: Creative Blogger