Dereva wa Bodaboda Akatika Mguu baada ya Kugongwa na Roli la Mizigo




Dereva wa pikipiki ya abiria maarufu kama bodaboda jina halijafahamika mpaka sasa (kwani hawezi kuongea) amepata ajali mbaya na kuvunjika kabisa mguu wake wa kulia mara baada ya kugongwa na roli la mchanga katika eneo la daraja la Mkolani wilayani Nyamagana nje kidogo ya jiji la Mwanza.
Kwa mujibu wa Mwandishi wetu aliyeweza kuwahi kufika ktk eneo la tukio na kutoa msaada wa gari kumfikisha dereva wa pikipiki hiyo aliyopata ajali Hospitali ya Rufaa ya Bugando, annasema kuwa dereva huyo alikuwa akitokea Mkolani kuelekea Buhongwa na Roli hilo lilikuwa likitokea Buhongwa kuelekea Mkolani, imetokea wakati dereva wa roli 'akiovateki' daladala iliyokuwa mbele yake ikibeba abilia, hivyo alipoipita tu daladala hiyo akakutana uso kwa uso na bodaboda.
Baadhi ya bodaboda na wasamalia wema wakimbeba majeruhi kumpeleka kwenye gari la MSD Kanda ya Ziwa ili kumkimbiza hospitali ya Bugando.
Hivi ndivyo mguu ulivyo vunjika baada ya kupata ajali.
Sambamba na kuvunjika mguu pia dereva huyo amevunjika vidole vitatu vya mkono wake wa kulia. 

TWAOMBA RADHI KWA PICHA HIZI 


Join Swahili One Community, "Like" and you will be one of us forever

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Copyright © 2013. swahili one Blog - All Rights Reserved
Customized by: Grace Tommy The One | Powered by: BS
Designed by: Creative Blogger