"Ingawa Tumetengana ila Mke wangu Namuheshimu" Bob Junior
STAA wa Bongo Fleva Rahim Nanji’Bob Junior’amefungukua kuwa ataendelea kumuheshimu mke mke wake Halima ally ambaye amezaa naye mtoto mmoja wa kiume hata kama wameachana.
Akifunguka kupitia mtandao wa instagram alisema kuwa ….leo tena jamani hakuna habari nyengine hata kama nimeachana nae kanizalia napaswa kuwekewa heshima mwanangu akija kuwa mkubwaa nita mwambia nini mimi inaniumaa bob junior tuu akilala akiamkaa ni bob junior kila sehemu…
Huku akipost sehemu ya gazeti la Amani iliyotoa stori hiyo huku habari kutoka kwa rafiki wa karibu na Bob Junior zinasema kwamba, ndoa hiyo ilivunjika muda mrefu lakini wahusika walikuwa wakifanya siri lakini Amani limeinasa.