Kiwanja cha Kombe la Dunia 2014 Brazil chaua watatu
Sao Paulo, Brazil - Vifo vya watu watatu vimeripotiwa kutokana na kuanguka kwa sehemu ya kiwanja kitakachotumika kwa ajili ya ufunguzi wa michuano hiyo mnamo siku ya Jumatano, November 27, huku ikielezwa kwamba ajali hiyo pia imesababisha uharibifu mkubwa.
Hii inamaanisha kwamba kutakuwa na ucheleweshwaji wa makabidhiano ya viwanja vyote 12 kwa FIFA itakapofika mwezi Desemba kama ambavyo imepangwa, hii ni kutokana na Uwanja huo wa Itaquerao kuanguka, mpaka inaanguka sehemu ya uwanja huo ulikuwa tayari umekamilika kwa asilimia 94.